Ajabu!! Mwanaume kukamatwa akiwa amevalia kaa mwanamke Lamu

Polisi katika eneo la Lamu walimkamata mwanaume mmoja akiwa amevalia kama mwanamke hii ni baada ya polisi kufikishiwa ripoti kuwa msichana ambaye ana tabia isiyo ya kawaida ameonekana.

Polisi walifikishiwa ripoti hiyo na chifu wa eneo la Langoni Haidar Fakii, Polisi wa NPS kaunti hiyo ya Lamu waliokuwa wakishikilia doria eneo la Kashmir.

Walifika katika eneo hilo, na kuenda katika nyumba hiyo na wakafanikiwa kumkamata mwanaume huyo aliyekuwa amevalia nguo za wanawake wa kiuslamu zinazo fahamika kama.

Baada ya muda usiokuwa mrefu Farida Chemutai alipatikana kuwa yeye si mwanamke hata bali ni mwanaume wa kutoka kaunti ya Makueni na jina lake ni Mutuku Nzambia wa eneo la Kithuku.

Mwanaume huyo amekuwa akitumia namba tofauti za simu ili kuwasiliana, zifuatazo ni namba ambazo amekuwa akitumia 0705 714 999 na 0773632242.

Aliwasili Lamu tarehe 11/3/2019 kutoka kaunti ya Nairobi, alidai kuwa alikuwa amealikwa Lamu na rafiki yake wa kike anayefahamika kama Zinab Wambua ambaye hadi sasa hajaweza kupatana na yeye.

Hakuweza kumuona wala kumguzishia macho alipo wasili katika eneo hilo la Lamu, kwa sasa Mutuku yuko katika kituo cha polisi kwa kuhojiwa zaidi na polisi hasa kwanini aliweza kubadilisha jina lake.

Na kwanini anavalia kama mwanamke ilhali yeye ni mwanaume.