Ajali inayohusisha magari manane yasabisha msongamano Nairobi

Jam Ngara
Jam Ngara
Magari manane Alhamisi asubuhi yalihusishwa katika ajali ya barabara ya Thika katika eneo la Kituo cha Polisi cha Muthaiga.

Ajali hiyo mwanzo ilisababishwa na mabasi mawili ya kampuni ya Virginia Coach na basi la Mwiki Sacco kabla ya magari mengine kuhusishwa.

Kamanda wa polisi katika kaunti ya Nairobi Philip Ndolo amesema kwamba basi la kampuni ya Virgnia iliteleza na kugonga  vichuma kando kando mwa barabara telezi kutokana na mvua kubwa unaonyesha.

"Kulikuwa kunayesha na mojawapo a mabasi likateleza barabarani...kisha basi la Mwiki Sacco likagonga hilo basi," Ndolo amesema.

Ndolo alisema kutokana na mvua kubwa,  hali ya barabara si shwari na madereva wameshauriwa kuendesha kwa utaratibu

Madereva wanaoelekea maeneo ya Ngara wameshauriwa kutafuta njia mbadala ili kuepuka eneo hilo la ajali.

Ndolo anasema kwamba hakuna majeruhi katika ajali hiyo.