Ajali ya gari 6 yaua abiria saba Kilifi. Yaliyojiri yasimuliwa

unnamed (5)
unnamed (5)
Idadi ya watu 7 wamefariki baada ya tukio la ajali kufanyika eneo la Makobeni, kaunti ndogo ya Kaloleni kaunti ya Kilifi.

Watu 6 wameaga papo kwa hapo na mwingine kukata roho katika hospitali ya Mariakani.

Kamanda wa polisi Patrick Oreri amedokeza kuwa watatu wamelazwa hospitali na majeraha kubwa.

“Hatuna idadi kamili ya watu waliopata majeraha kwa sababu kuna abiria tayari walikuwa washatolewa katika tukio la ajali na wakaazi wanaoishi karibu na sehemu hii." Amesema Okeri.

Okeri amesema kuwa dereva wa gari ya kibinafsi alikuwa anajaribu kuipita gari nyingine katika sehemu ya daraja iliyopo kwa mteremko.

Dereva huyu amepoteza mwelekeo na kugongana kichwa kwa kichwa na lori.

Tukio hili limepelekea kugongwa kwa matatu mbili kando na lori moja.

Mbunge wa eneo mbunge hilo William Kamoti amehuzunika na tukio hilo.

Aidha amedokeza kuwa alikuwa ameipa taarifa KeNHA orodha ya sehemu hatari katika barabara hiyo ili wajenge matuta ya kupunguza kasi ya magari.

“Tunawapa KeNHA siku 7 watengeneze matuta katika maeneo haya. Wasipofanya hivyo wanakijiji watachukua hatua." Alisema katika sehemu ya ajali.

Alikuwa ameandamana na naibu wa gavana  Gideon Saburi.

Moja kati ya matatu za Bambu Invest Limited Sacco yenye namba ya usajili KAP 907B imebondwa na kuharibika kabisa.

Idadi ya polisi kwa sasa ni 7 huku wakaazi wakitoa taarifa kuwa idadi ya watu 10 wamefariki.

Mabaki ya magari yaliyohusika katika ajali hiyo yalivutwa na kuhifadhiwa kituo cha Polisi cha Rabai.