Ajenda ya Ruto kupimana nguvu na Raila Odinga yaonyesha dalili za kufeli

vqruwvcpi0yzglkbkjc5c3b984685c15 (1)
vqruwvcpi0yzglkbkjc5c3b984685c15 (1)
Uchaguzi mdogo unaosubiriwa kufanyika katika eneo bunge la Kibra baada ya Ken Okoth kufariki utaonyesha na kupima nguvu za Kinara wa ODM na makamu wa rais William Ruto mwaka wa uchaguzi mkuu 2022. Siasa za eneo bunge hili zitawapa fahali hawa wawili nafasi kubwa ya kumenyana na kugundua nguvu zao hapa jijini Nairobi.

Soma hapa mengine:

Ingawaje hawahusiki katika kugombea moja kwa moja ila fahali hawa inaaminika kuwa kuna wakala wao katika zoezi hilo waliowatuma kuwakilisha. Uchaguzi huu utafanyika Tarehe 7 Novemba. Wachanganuzi wengi wa siasa aidha wanahoji kuwa huu utakuwa uwanja mzuri wa kuonyesha itakavyokuwa 2022.

“Uungwaji mkono wa Raila unapungua sio tu Kibra ama Nairobi bali ata nchi nzima. Mahasimu wake wa kisiasa, hususan Ruto atakuwa anajaribu kutingiza ubabe wa Raila. Iwapo atapata namba nzuri ya wafuasi,ataingia katika mchuano wa 2022 na nguvu imara." Mchanganuzi wa siasa Macharia Munene

Kiti hiki kilisalia pengo baada ya Ken Okoth kuaga. Ken alikuwa amechaguliwa kupitia tikiti ya chama cha ODM. Aliaga kwa maradhi ya saratani Julai 26 katika The Nairobi Hospital.

Soma hapa mengine:

Inadaiwa kuwa Ruto alijipenyeza katika uchaguzi huo kupitia uteuzi wa staa wa soka McDonald Mariga. Vyanzo mbalimbali vinakiri kuwa naibu wa rais alimpa presha Rais Kenyatta ili wateuwe mgombeaji. Uhuru hakutaka kushindana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kufuatia makubaliano yao ya Handshake Machi 9 2018.

Soma hapa mengine:

Aidha ajenda ya naibu wa rais kupimana nguvu na Raila Odinga inaonekana na dalili za kudumaa baada ya vita za ndani kwa ndani na mgawanyiko kugumbika chama tawala cha Jubilee kuhusu uteuzi wa fahali wake Mariga .