Akothee asimulia vile mwanasiasa maarufu alijaribu kumnyanyasa kingono

Akothee almaarufu rais wa mama wakulea watoto pekee aliweza simulia vile mwanasiasa maarufu aliweza jaribu kumnyanyasa kingono baada ya kuenda ofisini kwake kutafuta kazi. Ni jambo ambalo limekuwa likimsumbua hadi leo.

Aliweza kuongea kuhusu jambo hilo ili kuwaelemisha wakosoaji na watu hasa kwa wale huwa wana mkosoa na kumuhukumu kwa mambo ambayo yanaendelea katika maisha yake.

Akiandika katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram alisema....

"Ambacho mtoto wa kike anapitia katika ulimwengu wa giza ni mengi kuliko vile anapanua miguu hadharani,

"Baadhi ya viongozi wamekosa tabia ya kawaida wanatumia maofisi zao kuwanyanyasa kingono wasichana wadogo kwa manufaa yao,

"Wengine wameeka katika mawazo yao kuwa kitu cha maana ambacho wanaweza kwa mwanamke ni ngono,

"Wasichana ambao wamesoma wamo hatarini kuliko wale tayari wako katika vilabu na"disco" kama mtaanza kuvamia nafasi yetu kama wanawake tutaeka wazi vitendo vyenu," Alieleza Akothee.

Akothee hakuweza kutia kikomo bali aliongeza na kusema..

"Mwaka wa 2005 nilienda kutafuta kazi ata kama ni ya kufagia kwa ofisi ya waziri fulani, nilipatana na yeye kupitia kwa rafiki yangu ambaye tunaenda kanisa moja na yeye,

"Kila wakati niliweza kuenda katika ofisi yake, na nilikuwa wa mwisho kuhudumiwa ningekaa katika maeneo ya mapokezi, nikimgonja angeenda kukula chakula cha mchana kwa muda wa masaa matatu,

"Nilikuwa mvumilivu na sikuchoka, kila siku ningedhani hiyo ndio siku yangu, baada ya kuenda kwa wiki mzima, niliweza kumuona saa mbili usiku,

"Wakati kila mtu alikuwa ameenda kwa maana aliweza niambia nibaki nyuma,

"Niliweza ingia katika ofisi yake, nilimuelezea hadithi yangu, kisha nilimpa vyeti vyangu vya kidato cha nne kwa maana hivyo ndivyo vilikuwa na jibu,

"Wewe una kipaji msichana mrembo!! kisha alisema ataweza kunibeba, tulienda katika gari lake la Mercedes-Benz na kisha tukaenda," Akothee alisimulia.

Akothee alivyofikiria mambo yake sasa yako sawa alisema kuwa mwanaume huyo alianza kumshika bila adabu.

"At about the round about of integrity center, he took his ugly fat hands and put them on my thighs pulling my dress up🙄🙄,

"I grabbed his hands and threw it back to him🙄🙄 , he felt offended and put the car besides the road at community and kicked me out of his car 🙄🙄.

"It was dark in the middle of nowhere , whatever happened………… MORALS, he didn’t  care whether I got raped, killed, murdered ! .

"I only  had 20 Bob with no phone so there was nothing for thieves, But this was somebody daughter , someone’s mother , some rolemochieth kind of sh*t @veshashillan @rue.baby @fancy_makadia,” Aliandika Akothee.