Ali Kiba azungumzia taarifa za kumtema mkewe Amina Khalef

taDk9kqTURBXy8zNWMxMWViMjQxZTdlMjE1ZmIxMGFhZjY5YjAzZTBjMy5qcGVnkpUDADXNAtrNAZuTBc0DFM0BvIGhMAE
taDk9kqTURBXy8zNWMxMWViMjQxZTdlMjE1ZmIxMGFhZjY5YjAzZTBjMy5qcGVnkpUDADXNAtrNAZuTBc0DFM0BvIGhMAE
Staa na nyota wa Bongo Fleva Ali Kiba amefunguka kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake Amina Khalef.

Kiba amekana taarifa zilizokuwa zinagongwa vichwa vya habari kwamba amemtema mke wake.

Mapema wiki hii, runinga ya East Africa iliripoti kuwa staa huyu alikuwa amempa mkewe talaka 3.

“Msanii Ali Kiba amempa talaka tatu mkewe Amina Khalef  raia wa Kenya baada ya kushindwa kupata muafaka kuhusiana na ugomvi wao na ndugu wa Alikiba na Mama wa Alikiba… ,” Taarifa ya East Africa TV ilidokeza.

Kwa mujibu wa taarifa za East Africa TV, Ali Kiba alifikia uamuzi wa kumpa talaka mkewe baada ya kushindwa kufikia suluhu mwafaka.

Wanandoa hawa wameishi katika songombingo za mahusiano kwa kipindi kirefu.

Soma hadithi nyingine;

Ali Kiba aliteka vichwa vya habari kwa kuoa nchini mwanadada Amina Khalef.

Matatizo yanakisiwa kuanza katika familia.

Changamoto kuu zikiwa ni kuishi na familia kubwa ya staa huyu.

Katika mahojiano na chombo cha habari Tanzania,

Kiba amekana taarifa hizo,

“Sijaachana na mke wangu kama ambavyo watu wanadai bali nimemruhusu aende kwao nchini Kenya kufanya kazi." Alijitetea Kiba

Soma hadithi nyingine;

Aidha, Kiba amekana taarifa kuwa kuna mzozo baina ya Amina na mamake,

“Mama yangu hahusiki kabisa katika ugomvi huu na mama ndio mtu pekee ambaye alikuwa anatusuluhisha kwamba jamani malizeni haya mambo..."

Kiba alisimulia jinsi mamake anavyokwazika kusikia uvumi huo,

"Anaposikia watu wanavyomzungumzia hivi najisikia vibaya sana na hata mama yangu hayuko sawa mpaka sasa hivi kutokana na haya maneno..."

"Tuwaheshimu wazazi wetu jamani ukiona mtu anaongea hivi ujue hajafunzwa vizuri na wazazi wake."