Alichokisema Obama kuhusu Eliud Kipchoge, Eliud aomba wakutane

hH6k9kpTURBXy9lNWRkZTdlZDQ4MjRhZDJiZTQ2YWYyNjIyNmRkMThiMC5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB__1571046711_77502
hH6k9kpTURBXy9lNWRkZTdlZDQ4MjRhZDJiZTQ2YWYyNjIyNmRkMThiMC5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB__1571046711_77502
Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama ametoa tamko la ushindi na kuunga mkono ushindi wa Eliud Kipchoge.

Kupitia mtandao wa Twitter, Obama amesifia ushindi wa wakenya hawa wawili.

"Hapo jana (Jumamosi), Mkiambiaji Eliud Kipchoge amekuwa wa kwanza kuvunja rekodi ya masaa mawili. Hii leo (Jumapili)  Chichago, Brigid Kosgei ameweka rekodi mpya ya kidunia ya wanawake....Wawili hawa ni mfano mzuri wa uwezo wa binadamu kufaulu..." Obama

Kama Eliud Kipchoge, Obama mwenyewe alitoa motisha kubwa zaidi kwa dunia baada ya kuchaguliwa kuiongoza Marekani.

Eliud ameingia katika historia ya binadamu wa kwanza kumaliza mbio za kilomita 42 kwa masaa mawili.

Kwa sasa Eliud anaomba kukutana na Obama baada ya pongezi hizo.

"...Ahsante kwa maneno yako ya busara. Kwa haya maisha huwa tunaishi kuwapa moyo wengine. Ningefarijika zaidi iwapo tungekutana na tujadili jinsi tunavyoweza kufanya ulimwengu huu uwe wa kukimbia..." Eliud alimwandia Obama katika Twitter.

Haya yanajiri baada ya Eliud Kipchoge kutwaa ushindi mkubwa katika mbio za Marathon mjini Vienna, Austria.