Alivyokuwa ananipindua,Mashallaah!,nakosa sana penzi lake

NA NICKSON TOSI

Muigizaji wa filamu za Tanzania Jacqueline Wolper amefunguka na kudai kuwa anakosa sana penzi la Harmonize aliyekuwa mpenzi wake kwa wakati mmoja.

Katika ujumbe wake alioutuma kwenye mtandao wake wa instagram ,Wolper alikiri kuwa amepitia mengi tangu walipotengana na  Harmonize ikiwemo penzi lake hatari la lililokuwa linamfanya kuwa kichaa,na kuongeza kuwa kuzinduliwa kwa albamu ya nyimbo za mziki na msanii huyo ni kitu cha kujivunia.

Aliongeza kuwa anatamani sana kurudiana na msanuii huyo kwani kisima chake cha asali kimefanya butu kwa sababu hajapata mtu wa kumpa mikiki mikali kama alivyokuwa anampa Harmonize.

Nachukua Nafasi yakukutakia  Mema kwenye uzinduzi wa albamu yako leo . Nakumbuka ilikua ndoto  yako na hatimaye umekamilisha,Tumetoka Mbali Tumepitia Mengi Tumegombanishwa sana yote Ni sababu ya kiburi changu ,lakini kwa yote  ukweli sifichi kwakua siwezi acha kufurahia unachofanya naunavyopambana..Hakuna mahusiano kati yangu na wewe lakin imani yangu inanituma kwa kuwa nakujua Na mimi najijua Najua kila mmoja anaumia kwa nafasi yake kutokuongea Na mwenzie,” alisema Wolper.

Wolper alikiri kuwa amekuwa akijaribu kumfikia Harmonize na lengo la kutaka kurutiana naye  bila ya kujali yale watu watasema katika mitandao ya kijamii .

Aliongeza kuwa dhamira yake si kuharibu ndoa ya Harmonize na mkewe Sarah.

“Nathubutu kusema maumivu yapo na hayajifichi hata Nizuge vipi ukweli unaujua wewe Rajabu Na Mimi Khadija 😭Huku insta watanitukana kwa haya niliyoandika kama wolper . Kama khadija naumia mwenyewe na hakuna wakunisaidia. 😭🙏 Katika huu ujumbe sina maana yoyote mbaya ya kuaribu mahusiano yako wala yangu ila nimekua huru kuongea ili nililotaka kuongea live mbele yako. aliandika  Wolper.