Aliyekuwa Rais wa Ufaransa Jacques Chirac aaga dunia

chirac france
chirac france
Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac ameaga dunia akiwa na umri wa 86.
Alifariki Alhamisi asubuhi akiwa na familia yake, mwanawe wa kambo alieleza shirika la Reuters.
Chirac alihudumu kama rais kati ya mwaka wa 1995-2007. Katika kipindi cha uongozi wake, alifanya mageuzi mengi pamoja na kuunganisha mataifa ya Ulaya kutumia sarafu moja na kufutilia mbali sheria iliyowalazimu raia kuhudumu katika kikosi cha jeshi.
Pia alipunguza muhula wa rais kuhudumu mamlakani kutoka miaka 7 hadi miaka 5.

Rais huyo wa zamani anakumbukwa pia kwa kupinga vikali Marekani ilipovamia Iraq mwaka wa 2003.
Baada ya kutawala nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 12, Jacques Chirac alikumbwa na kashfa nyingi za ufisadi. Alishtakiwa mwaka wa 2011 kwa makosa ya ubadhirifu wa fedha alipokuwa akihudumu kama Meya.
Bunge la Ufaransa limempa kiongozi huyo heshima ya dakika moja kwa kunyamaza.