Aliyemnyofoa sehemu za siri mmewe ashtakiwa. Ripoti yachapishwa kuhusu afya yake ya akili

unnamed
unnamed
Mwanamke aliyeshtakiwa kwa tuhuma za kunyofoa sehemu nyeti za mmewe amepata hukumu ya kufanya mauaji jana katika mahakama ya Nakuru.

Kwa mujibu wa mahakama hiyo, uchunguzi wa kina wa afya ya akili ya Naomi Nyokabi uliofanywa kwa utendeti katika hospitali ya Nakuru Level 5 unaonyesha kuwa yuko sawa kusikiliza mashtaka.

Soma hapa;

“Ripoti inaonyesha bayana kwamba mshtakiwa ana akili timamu na anaruhusiwa kusimama kizimbani kusikiliza kesi dhidi yake." Alisema jaji Joel Ngugi.

Aidha Nyokabi alikana mashtaka. Naomi anashtakiwa kukata sehemu za siri za mmewe ambaye baadaye alifariki akiwa katika hospitali ya Nakuru Level 5. Ripoti zinasema kuwa mmewe Nyokabi aliaga baada ya kububujikwa na kiasi kikubwa cha damu.

 Ripoti za polisi zinaonyesha kuwa mkewe alipiga kwa rungu kabla ya kuchukua kisu kikali na kunyofoa sehemu zake za siri. Nyokabi alinusurika kichapo cha umati baada ya polisi kufika na kumkamata.