IMG_0121__1571067011_77368

Aliyepata alama 428 KCPE afanya kazi ya ‘walking scarecrow’ kwa shamba ya ngano

Dkt. John Karanja alifunguka mwanzo mwisho kuhusu maisha yake katika kitengo cha Ilikuaje Bustani La Massawe.

John amesimulia jinsi alilelewa katika familia iliyokumbwa na ukata mwingi.

Kwa sasa ndiye Inspekta wa polisi katika huduma ya Jela nchini na ameweza kusoma sana hadi kufikia hadhi ya Dkt.

Ni msomi,mwandishi na kasisi anahimiza watu kufanya vizuri ili kufikia kiwango  hicho amepitia mengi.

Alitaka awe Daktari ila kulingana na umaskini uliokuwa kwao, jamaa huyu alipata tabu kubwa.

Alichokisema Obama kuhusu Eliud Kipchoge, Eliud aomba wakutane

 “Nimezaliwa pande ya Nyeri. Wazazi wangu walikuwa maskini sana. Babangu aliaga…. Mama akaachiwa kazi ya kufulia watu nguo.” alianza John

“Nilikuwa msomi Darasani. Mama alikuwa anafua nguo ili kutusaidia. Karo yangu ikawa haipo baada ya kupata alama 428 za KCPE…”

“Hapo nikafanya mungu awe rafiki wa karibu na nikaanza kutembea na Mungu…”

John alitafuta kazi ya kwanza ili apate kuwekeza karo,

“Nilikuwa na miaka 14 nikapewa kazi ya kufunga ng’ombe na mbuzi…Nilipata alama 428….Mama alisema nikubalie wale wengine wasome wajue kusoma vibango.”

Kazi hii ilimchosha na akaamua kutafuta kazi kwingine,

“Nikatoka Othaya nikaenda Mweiga nikafute kazi kwa Baba Luka. Nikawa nawekeza ili nipate karo ya kusomea udaktari…’

Mkimbia uchi usiku asimulia siri za familia anazotembelea,ajisifia kwa mbio

“So Massawe nikawa maid kulea watoto wawili nikitafuta karo… Nalipwa pesa 450 kila mwisho wa mwezi….”\

Kazi hii aliaacha na akafuta kazi nyingine ya kuchunga shamba la ngano,

“Kufika Mweiga Town nikapata kazi ya kulinda shamba la ngano. Nikawa walking scarecrow kwa shamba ya ngano.”

“Nikalipwa shilingi 700 kwa mwezi…”

Kitambulisho kilimkosesha kazi nyingi zaidi huku waajiri wakihofia kumwajiri.

Hatimaye njia zake zilifunguka na akawa msomi na kwa sasa anasaidia wengi kujikimu kimaisha.

Photo Credits: Abraham kivuva

Read More:

Comments

comments