Aluta Continua: Ruto aendelea na mipango ya kuchukua usukani,aamua kukabiliana na Uhuru

ruto
ruto
Naibu wa rais William Ruto anatafuta chombo mbadala cha kutumia kuwania urais mwaka wa 2022 huku ishara zikionyesha uwezekano wa kuzuka  makabiliano makali  kati yake na rais Uhuru Kenyatta.

Kwa mara ya kwanza baada ya meizi kadhaa ya kuonekana kutengwa na washirika wake kulengwa,  Ruto siku ya Jumamosi alifunguka na kusimulia masaibu ambayo washirika wake wanayapitia serikalini na bungeni   katika kijembe aliochoonekana kumuelekezea mkuu wake, Uhuru .Uhuru  ametekeleza mageuzi makubwa katika uongozi wa mabunge yote mawili katika kilichoonekana wazi kama njama ya kukabiliana na ushawishi  wa Ruto kisiasa tunapoelekea uchaguzi mkuu wa 20222. Rais Kenyatta amewashtumu  Ruto na washirika wake kwa kuhujumu ajenda yake ya maendeleo na badala yake kuendeleza siasa za urithi.

Hatima ya Ruto katika chama cha Jubilee inaendelea kuwa katika hali ya mizani  na huenda anapanga kikakatai ya kujiondoa wakati ufaao ili kukitumia chama kingine kugombea kiti cha urais . Duru zaarifu kwamba  washrika wa Ruto wanazinghatia kukitwa chama  The Party of Development and Reforms (PDR).

PDR  kina ushawishi mkubwa miongoni mwa jamii za wafugaji wa kuhama hama  na  miongoni mwa vyama tanzu vya Jubilee . Kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2017  PDR   kilikuwa kikiendeshwa katika afisi ya Naibu wa rais  katika jengo la  Transnational Bank House  kwenye barabara ya  City Hall Way. Afisi hizo katika ghorofa ya tisa   zilikuwa zikitumiwa kama afisi ya kibinafsi ya naibu wa rais  tangu mwaka wa 2007 alipokuwa mbunge wa eldoret kaskazini . Duru zaarifu huenda chama hicho kikabilishwa jina  na kisha kuboreshwa ili kutumiwa na Ruto .

Baadye DP atafanya mikataba ya ushirikiano na vyama vingine  ili kujenga muungano thabiti wa kisiasa kukabiliana na mrengo ambao utaungwa mkono na rais Kenyatta pamoja na mshirika wake mpya kisiasa bwana Raila Odinga .

Wandani wanasema chama cha waziri wa zamani wa Kilimo Mwangi Kiunjuri  Service Party  na the  Transformational National Alliance  kinachohusishwa na mbunge wa  gatundu kusini  Moses Kuria vitakuwa katika muungano wa Ruto kwa matayuarisho ya uchaguzi mkuu wa 2022 .

The United Green Party (UGP)  na  Grand Dream Development Party (GDDP) pia ni baadhi ya vyama ambavyo Ruto analenga kushirikiana navyo katika mpango  huo wake. Kuna mikakati pia ya kuwashawishi Musalia Mudavadi wa ANC na Moses Wetangula wa Ford Kenya kujiunga na mrengo wa naibu wa rais .Chama cha PDR kinatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni kwa lengo la kukipa umaarufu .tayari chama hicho kipo katika mkataba wa ushirikiano na chama cha  Jubilee .