Amani nchini ni bora kuliko ndoto zangu za urais, asema Ruto

unnamed__1576841828_21284
unnamed__1576841828_21284
Naibu wa rais William Ruto amesema kuwa amani ya Kenya ni bora zaidi kushinda ndoto yake ya kuwa rais mwaka wa 2022.

Ruto aidha amedokeza kuwa hataki kuwa sababu ya umwagikaji damu unaotokea kila baada ya uchaguzi.

 Naibu wa rais alikuwa akihutubu katika eneo la Sugoi kaunti ya Uasin Gishu.

Haya yanajiri huku mirengo mbili ya chama cha Jubilee ikionekana kutofautiana kwa swala la atakamrithi rais Kenyatta.

Kuna mrengo wa kieleweke ambao unapigiwa debe sana na mbunge wa zamani wa starehe Maina Kamanda na mbunge eneo la mji wa Nyeri Wambugu Ngunjiri .

Tanga tanga kwa upande mwingine wameonekana kumpigia debe naibu wa Rais William Ruto, wakisisitiza kuwa naibu huyo atawania kiti cha urais mwaka wa 2022, baada ya Rais Kenyatta kumaliza muhula wake.

Mrengo huo wa Tanga Tanga unaongozwa na mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung'wa na mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro na baadhi ya wengineyo.