Amina Khalef kumroga Sameer, Ali Kiba amrudisha mkewe Kenya

unnamed
unnamed
Ali Kiba amekiri kuwa ndoa yake na Amina Khalef ipo katika wakati mgumu na kuwa inakumbwa na matatizo tele.

Katika mahojiano, Ali Kiba ametangaza bayana kuwa mkewe amerudi nchini kutoka Tanzania.

"Ni ukweli kuwa mimi na bibi yangu tuna matatizo, na hili ni jambo la kawaida kwa wanandoa..."

Soma hadithi nyingine;

"Nilimrudisha kwa wazazi wake Kenya. Nilitaka pia yeye afanye kazi halafu nikasafiri Uropa."

" Hapo mwanzoni alikuwa amenitaarifu kuwa angependa kufanya kazi kwa sababu amesoma sana.

"Nilipotoka Uropa akaniambia yuko poa na nina ruksa ya kuenda kumwona kwao."

"Sijampa talaka mwanzo ila kitu mtu anafanya ya kwake. Talaka sio kitu cha kusifia au ata cha kutangazia watu."

Kiba alisema kuwa mamake alikuwa wa msaada sana kuwaleta pamoja.

Soma hadithi nyingine;

"Ukweli ni kuwa hapo mwanzoni tulikuwa na hali ya kutoelewana ila mama akasuluhisha."

Ubuyu wa Tanzania unaenea kuwa Amina alishukiwa kwa tuhuma za uchawi taarifa na ambazo Kiba alikana.

"Sio kweli walivyosema kuwa Amina hapendi watu. Kulikuwepo na tetesi kuwa mke wangu anatumia ushirikina kwa mtoto wangu Sameer..."

"Hilo lilinishangaza sana," Alisema Kiba.

"Mahasidi wangu wanadhani kuwa watanishusha. Sitaishi maisha ya mitandao ya kijamii. Sipendi kuingilia maisha ya watu."

Soma hadithi nyingine;

Aidha Kiba alisema kuwa ana ruksa ya kuoa wanawake wengi.

"Wakati mke wangu anaponikasirisha na naamua kumuacha, hilo ni jambo la kawaida. Naruhusiwa kuoa mpaka wanawake wanne."