Amri yatolewa, afisa serikalini akiomba rushwa, Mpige risasi

143930d2_8684_11e9_a9bc_e8ed9093c066_image_hires_142623__1569314595_56187
143930d2_8684_11e9_a9bc_e8ed9093c066_image_hires_142623__1569314595_56187
Iwapo kiongozi yeyote nchini Ufilipino atapatikana katika hali ya kuitisha hongo, afisa huyu anapaswa kupigwa risasi.

Hii ni kwa mujibu wa Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte .

Rais huyu amesema kauli hii katika juhudi za kukomesha ufisadi miongoni mwa maafisa seikalini.

Akitaja ufisadi kama kisiki cha maendeleo, Rais Duterte amekashifu kitendo cha ulaghai katika ngazi kuu serikalini.

Soma hadithi nyingine:

Duterte alikuwa akihutubia raia wa nchi hiyo katika jimbo la Bataan nchini humo.

Rais wa Ufilipino ni dikteta.

Ametangaza kuwa yuko tayari kusimama kizimbani iwapo afisa mmoja wa serikali atapata jeraha la risasi.

Soma hadithi nyingine:

"Kiongozi wa serikali yangu iwapo ataomba rushwa, mpige risasi ila usimuue mjeruhi tu..."

"Mimi najua taifa la Ufilipino limekwamishwa na ufisadi..."

"Narudia mwananchi unayemiliki bunduki,kiongozi atakayeomba rushwa mpige risasi." Alisisitiza rais huyo

Soma hadithi nyingine:

Rais huyu anatajwa kuwa katili na dikteta.

Aliwahi kufanya msako wa wahalifu na wauzaji dawa za kulevya na kuwaua wote.

Aidha, Rais huyu aliwahi kushika kasi katika mitandao ya kijamii kwa kumkejeli muumba wake.

Alimkejeli Mungu kwa kumuita "Mpumbavu" kwa kumuumba Eva na Adamu huku akiwapa masharti ambayo hayawezekani.