Anatoka Rwanda – Maelezo yafichuka kuhusu mwanamke amabaye Diamond anapanga kufunga ndoa naye

Diamond Platnumz  amehusiswa na wanawake kadhaa tangu kuvunjika kwa uhusiano wake na  Tanasha Donna  na hadi sasa hajathibitisha yupo katika uhusiano na mwanamke yupi .

Kuna uvumi unaozagaa kwamba Diamond anapanga kuoa hivi karibuni lakini ni wachahe sana wanaomjua Bi harusi mtarajiwa kwani jambo hilo limewekwa  kwa usiri mkubwa na familia yake .

Wakati Diamond alipoishuhudia harusi ya dadake Esma ,palizuka tena uvumi huo kuhusu harusi ijayo ya Diamond  na kwamba mazungumzo ya kulipa mahari yamepiga hatua

Aliyepasuambarika ni mkuu wa zamani wa mkoa wa Dar  Paul Makonda  ambaye inaripotiwa anaongoza mazungumzo ya kulipa mahari .

Duru zaarifu kwamba mwanamke huyo ni kutoka familia ya kifalme  nchini Rwanda  na kwamba familia yake ni ya kitajiri sana  . Inadaiwa Diamond na mwanamke huyo wamekuwa wakionana sasa kwa miezi sita .

Makonda,  ambaye alikuwepo pia wakatyi wa harusi ya Esma alisema ;

“Mama (Mama Dangote) ulinipa kazi na kazi hiyo sio rahisi ni ngumu ila nakuhakikishia mwezi wa nane tunaenda kutoa mahari ya Diamond. Tushakubaliana, tumesharidhia kwa mke ambaye nimemwona mimi. Sio wale wanaosema “wao” a-a-ah. Nilimwona nikampitisha. Kwa hiyo Esma umetufungulia njia, kakako anafuata.”

Mwezi huu ndio makataa ya kukamilisha mazungumzo hayo ya mahri  kabla  ya mwanamke huyo kuleta Tanzania .

“Nina imani mwezi wa nane huu tukikamilisha. Tulikuwa na mpango tufanye mambo yaende haraka. Lakini mwezi huu (Agosti) tunaenda kutoa mahari.”

Swali ni je ,hizi ni sarakasi za Diamond ambazo amemuingiza ndani Makonda kama muigizaji ama kweli kuna mwanamke njia ama harusi inaynukia?muda ndio utakaosema ukweli na hamna uchungu wa kungoja ili kushuhudia