'Angeficha kondomu zilizobaki chini ya kitanda,' Akothee azungumzia mapambano ya uchumba

Msanii Akothee amesimulia jinsi wanawake walikuwa wanamuonea gere alipokuwa mpenzi wa Papa Ojwang huku wasijue kuwa ailkuwa anapitia chagamoto kibao.

Huku wengi wakimfahamu kama Papa Ojwang, angeenda kujivinjari huku akumuacha Akothee akiwa mjamzito huku asijue la kufanya wala kutenda.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii Akothee alisema mapito hayo yalimfunza mengi;

"Wanawake wengi walikuwa wanaionea wivu baada ya kuwa na papa Ojwang hawakujua usiku sikuwa napata usingizi nilikuwa natamani tu anishike mkono nilipokuwa naenda kununua vitu Nakumatt mmm

Mtoto wangu angetembea mita kumi mbali nami baba yake hakuwa nyumbani wakati wote, alikuwa anafika nyumbani saa nane alfajiri hata baada ya kumpikia na kumpa JB🙄😭😭😭,

Mwanamume huyo angetoka nyumbani saa tano usiku na kusema anaenda kunywa vileo katika klabu cha safari inn."

Akothee alisema kuwa siku moja aliamua kufuata mumewe ili kujua alichokuwa anafanya, alipigwa na butwaa alipomfuata na kumuona ameingia kwa mwanamke mwingine.

"Siku moja niliamua kumfuata, alikuwa anaendesha gari nililokuwa nimempa, alipowasili mtwapa aliegesha gari kwa vichochoro sikujua aliingia kwa nyumba gani

Nashuku ni nyumba ya mwanamke ambaye angezungumza naye sana aliyefahamika kama 'Amore' lakini walikuwa wengi sikujua haswa ni yupi

Nilikata tamaa na nikaamua kurudi nyumbani kwa maana hapakuwa pahali pazuri pa kuegesha gari na nilikuwa mjamzito wa miezi sita."

Alizidi na usimulizi wake,

"Nilirudi nyumbani na ulimi wangu ukiwa umekauka, shingo ndefu na tumbo tupu, alirudi nyumbani saa kumi na moja asubuhi na ningemsikia anaficha kitu chini ya kitanda

“WARARARARARA ” sauti ya kondomu, niliamka asubuhi nikamwambia nataka kipochi chake nichukue pesa ili nikanunua bidhaa za nyumbani kwa maana alikuwa anakula hapo na kuishi hapo pia

Ulikuwa tu uongo nilikuwa nataka kwenda chini ya gongoro ili kuthibitisha hofu yangu, alinionyesha mahali sauti ya Wararara ilikuwa inatoka, nilipata fursa ya kuthibitisha hofu yanugu

Niliposhika ilikuwa ni kondomu ambayo ilibaki kutoka kwa kitendo cha awali, nilisikia ni kama mtoto ananisukuma atoke."