Uchunguzi uliofanywa na mashirika mbali mbali ya vyombo vya habari na kueteta haki za binadamu umeonyesha kwamba nyingi ya mali inayomilikiwa na Bi Dos santos ilipatikana kwa njia isio halali na iliyozidi kuwafilisi wananchi wa Angola . Kuna pengo kubwa zaidi kati ya watu maskini na matajiri nchini humo na mafanikio yaliyoletwa na uchimbaji mafuta na pato la madini haujaweza kuwatiririkia raia wa kawaida nchini humo.
Hilo limelaumiwa kusababishwa na ubinafsi na ulafi wa watu wenye maamlaka na uwezo wa kupora mali ya umma bila kuogopa matokeo yoyote kama vile Bi Isabel. Mojawapo ya wizi mkubwa sana uliotekelezwa nchini Angola ni kupitia kwa kampuni moja iliyosimamiwa kutoka London yenye uhusiano na kampuni ya mafuta ya Angola Sonangol.Bi Isabel alipewa jukumu la kuisimamia kampuni hiyo mwaka wa 2016 kwa sababu ya agizo la rais , babake Jose Eduardo Dos Santos ambaye aliiongoza nchi hiyo kama mali yake kwa miaka 38 . Lakini babake alipostaafu mwaka wa 2017 ,nafasi ya Isabel katika kampuni ya Sonangol ilikuwa hatarini na muda mfupi baadaye alifurushwa kutoka nafasi hiyo na rais mpya Joao Lourenço ambaye pia ameamua kuitwaa mali ya baadhi ya watu wa familia ya mtangulizi wake . Raia wengi wa Angola wameshangazwa kutokana na jinsi rais Joao Lourenço anavyokabiliana na uha,lifu uliiotekelezwa na watu wa familia ya mtangulizi wake .