Arushia mtu kemikali na kuchana mbuga, Kelvin aelezea kuhusu hasimu asiyemjua

70506865_367945557428840_2358638972009185280_n_3___1568638520_96530
70506865_367945557428840_2358638972009185280_n_3___1568638520_96530
Kelvin amesimulia jinsi mtu asiyejulikana mpaka leo alibeba mkebe wa kemikali na kummwagia usoni.

Kelvin alikuwa anasimulia katika kituo cha Jambo kitengo cha Ilikuaje Bustani la Massawe Jappani.

Kwa sasa, kitu na ambacho kinamkosesha usingizi ni kumfahamu aliyefanya  kitendo hiki.

"Nilikuwa natembea mtaa wa Nanyuki. Nilikuwa naenda kazini saa kumi na moja asubuhi. Taa za stima zilikuwa ishajizima saa 5...Kuna mtu alikuwa ananisubiri pale..Kufika pale ule mtu atokelezea akanimwangia kitu kama maji na akatoroka."

Soma hadithi nyingine;

Ubaridi wa asubuhi ulimfanya ahisi kana kwamba mtu kamrushia maji ila ghafla akaanza kuchomeka mwilini.

"Baada ya sekunde kadhaa kile kitu kikaanza kunichoma...Mwili mzima ukaanza kudunga kama sindano...Kushika nguo zangu zikararuka."

"Nikaita Gate Man nikamwambia nipeleke pahali kuna mfereji."

Pale akajipa huduma ya kwanza na kuanza kufikiria ni jinsi gani atakavyoweza kufika hospitali

Soma hadithi nyingine;

"Bado ilikuwa inanichoma...Nilikuwa naona moshi peke yake...Nikaona niende hospitali...Nikapigia rafiki yangu akanipeleka Nanyuki Refferal Hospital."

Jamaa huyu anasimulia kuwa madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya Nanyuki hawakuchukulia hali yake kama ya dharura.

"Daktari hakuichukulia kama Emergency. Akanidunga sindano mbili kisha akaniambia ningoje daktari mwingine aje."

Baadaye jamaa huyu alipiga ripoti katika kituo cha polisi ili waweze kubaini mtu aliyefanya kitendo hicho.

"Nikaamua kwenda Nanyuki Police Station...Wiki za kwanza mbili nilikuwa sioni...Uso wangu ulikuwa unatoka usaha. Ilikuwa uchungu sana. Damu ilikuwa kumwagika."

Soma hadithi nyingine;

Aidha, Kelvin aliipoteza kazi yake. Anasema kuwa bibi yake amekuwa wa msaada mkubwa tangu matatizo haya yawepo. Hali kadhalika uchunguzi wa kamera za CCTV haujaweza kuleta taswira kamili ya hasidi wake asiyemjua.

"Wakati tuliangalia kwa CCTV kamera. mtu alikuwa amejifunika uso na hatungemtambua...Baada ya wiki nikawa naenda kliniki. Nilikuwa naongea ila singeongea kwa muda.Kupumua ilikuwa shida."

Soma hadithi nyingine;

Baadaye Kelvin amesema kuwa yuko sawa baada ya matibabu na kukubali yaliyotokea.

Kelvin anamsifia mkewe na watoto wawili kwa kuwa mwaminifu wakati huu wote wa matatizo.