Aukot amkosoa Raila kuhusu "punguza mzigo"

Kiongozi wa Third Way Alliance Ekuru aukot amewakashifu wanasiasa wanaopinga mswada wake wa punguza mzigo na kuwataja kama walionufaika na ufisadi.

Aukot alisema viongozi kama hao wanataka wakenya kusalia katika hali ya ufukara ili waendelea kuwatumia kisiasa kwa manufaa yao ya kibinafsi. Asema kinara wa ODM Raila Odinga, kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale, Seneta wa Bungoma Moses Wetangula na Kalonzo Musyoka wa Wiper wanapinga mswada wake.

Soma pia:

“Wamenukuliwa wakiambia wakenya kukakata pendekezo la Punguza mzigo tukisubiri pendekezo la Ongeza mzigo,” Aukot alisema.

Akizungumza katika City Hall siku ya Jumatano alipokuwa akiongoza vikao vya uhamasisho kuhusu mswada huo, Aukot alisema mswada wake unalenga kuimarisha nguvu za wakenya ili kuhakikisha kila mmoja anapata huduma sawa za serikali.

“Kwa njia hii tutapunguza uhasama wa kisiasa na hata upinzani,” alisema.

Soma pia:

Aukot alisema wakati umewadia kwa wakenya kuungana na kukataa viongozi wanaowatumia kama vyombo vya kupiga kura, na kisha kuwatelekeza.

“Watu wa Kenya wanahitaji maendeleo, sio siasa za ubinafsi,”alisema.

Aukot alimbia viongozi kuacha kudunisiha harakati zinazolenga kuimarisha maisha ya wakenya wote.

“Haya si mashindano ya kisiasa na unafaa kuacha kucheza siasa na maisha ya wakenya,” alisema.

Alimuonya Duale kwamba vitisho vyake dhidi ya wakilishi wadi ni hatia na kuzitaka idara za DCI na DPP kuanzisha uchunguzi na kumchukulia hatua za kisheria.