Avuna pakubwa ! Afisi ya Raila Odinga kuanza kupokea shilingi milioni 72 kutoka kwa hazina ya kitaifa

NA NICKSON TOSI

Kinara wa ODM Raila Odinga sasa ataanza kukulia pakubwa baada ya hazina ya kitaifa kutenga shilingi milioni 72 zitakazotumika katika afisi yake ambazo zitatumwa rasmi kama aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya.

Hata hivyo, Raila na Kalonzo Musyoka watasubiri kwa muda kabla ya kupokea malipo ambayo walikuwa wanapata wawili hao walikuwa wanapokea malipo ya uzeeni ambazo kwa mujibu wa bajeti zilikuwa bilioni 1.5

‘ Iwapo mtasitisha shughuli zote nchini, peeni watu chakula’ -Raila asema

Wafanyakazi katika afisi ya Raila pia wametengewa shilingi milioni 10 kama za mishahara yao.
Tangu kutoka kustaafu kama waziri mkuu mnamo mwaka wa 2013, Raila amekuwa akiirai serikali kumlipa marupurupu yake kama viongozi wengine akiwemo rais mstaafu Mwai Kibaki ambaye bado anapokea malipo ya uzeeni kutoka kwa serikali.
‘Corona cannot stop Reggea!’ Raila Asema
 
Kibaki amekuwa akipata milioni 3 kama malipo ya uzeeni kila mwaka huku mahitaji yake ya kibinafsi kama matibabu yakisimamiwa na serikali.
Kiingereza balaa, matusi namba one! Sudi amtaka Raila aende Nigeria kuleta dawa ya Corona
Ni mara ya kwanza sasa afisi ya Raila Odinga inatengewa kima hicho cha pesa tangu rais Uhuru Kunyetta kuchukua uongozi nchini.
Mwanzo kiongozi wa taifa alikuwa ameshinikiza Kalonzo na Raila kustaafu kutoka kwa siasa ndiposa waanze kupata malipo hayo