Baba na mwanawe wafungwa miaka 15 kwa kumnajisi mwanamke -Nakuru

HANDS-TIED
HANDS-TIED
Mzee wa miaka 58 na mwanawe wa kiume miaka 28 wamefungwa miaka 15 gerzani kila mmoja baada ya kupatikana na makosa ya kumnajisi mwanamke ambaye alikuwa jirani yao.

Hakimu wa mahakama ya Molo Emmanuel Soita amesema mashtaka yaliwasilisha mbele ya mahakama na John Limo yalionyesha namna John Chirchir na mwanawe Vincent Lang'at walivyotenda kitendo hicho mnamo Juni 27,2018 ,wakitekeleza unyama huo katika kijiji cha Telowa ,eneobunge la Kuresoi Kaskazini ,kaunti ya Nakuru.

Walioshuhudia kitendo hicho wamesema Chirchir na Lang'ata walifanyia kitendo hicho katika nyumba yao kabla ya kumwachilia mwathiriwa.