Baba ni baba ata awe mchawi-Ujumbe wa Bahati kwa Harmonize

Msanii Kevin Bahati amemuomba msanii wa nyimbo za bongo Harmonize almaarufu Konde boy, aende na kumuomba staa wa bongo Diamond msamaha, kupitia ujumbe aliouandika kwenye mitandao ya kijamii mtoto wa mama alimsihi Harmonize anyenyekee na kuoba msamaha.

Alizidi na kusema kuwa makosa yake hayawezi kulinganishwa na moyo mwema ambao ulimfanya awe mtu wa maana katika maisha yake.

"Hoja yangu ni kuwa makosa yake hayawezi linganishwa na moyo mwema ambao ulimchukua mitaani na kisha kumfanya kujulikana na ulimwengu

Mungu alimtumia ili uweze kujulikana duniani, ninapomalizia mahubiri yangu, nenda ukanyenyekee omba msamaha na uende zako na baraka zako Bro- Unajua Baba Ni Baba ata Awe Mchawiii... Hivyo Baba anauwezo Wakubariki na Kulahani...

Kam wataka kuwa #Tembo mwenye huwa wasema, wachana na vita vya aibu nenda ukalete amani kati yenu,kuna siku #Wizkid alikuwa amesajiliwa na #Banky W na baada ya mkataba wake kukamilika bado huwa anatambua na kumpa heshima Banky W kama baba mwenye kuanzisha kibali chake cha usanii

Kumbuka KARMA ni ya ukweli, hivi karibuni wasanii ambao umewasajili katika lebo yako wanaweza kukufanyia kitendo hicho, Husinichukulie kwa ubaya, Harmonize wewe i rafiki yangu na kumbuka nilikusaidia wakati wowote ulipokuwa wahitaji msaada wangu

Fanya jambo bro!!!."Ujumbe ulisoma.

Bahati alizidi kunakili ujumbe wake na kumshauri Harmonize awache kuwa na ugomvi na Diamond bali aende na kuomba msamaha  kwa maana ni baba yake wa muziki wake.

Msanii huyo aliandika ujumbe huo huku akipost picha ya Harmonize na Diamond.

"Dini yangu inanifunza ni mheshimu baba na mama yangu, na kwa hivyo @ Wasafi ndio mama na baba yako, najua kauli ya sasa ni kuwa na ugomvi na mtu aliyefanikiwa ili nawe ufanikiwa kwa haraka ili huwe juu na lakini si amini kwa hilo Bro!!!

Tunaweza fahamika bila la kuleta ugomvi, Bro haupaswi kuwa na ugomvi na Diamond ili huwe juu yake wahitaji baraka zake Ndio pia Usitumie hizi Nguvu Nyiingiii ku Prove a Point. Every One has their Faults and I Believe your Boss is not a Perfect Man; Ata Mimi amenikosea, Aliwachana na Sister Wa Mine but Sahi Niko Kwa Maombi Warudiane🙏." Aliandika Bahati.