Baba wa walemavu apokea nyumba ya Rais iliyokataliwa

charles Macharia
charles Macharia
Ni furaha aliyokuwa nayo mwanaume 58, na bali hakuweza kuficha furaha yake kwa kupewa nyumba iliyokamilika na rais Uhuru Kenyatta, hii ni baada ya familia ilyokuwa imejengewa nyumba hiyo kuikataa.

Katika sherehe ya kupeana nyumba hiyo iliyotayarishwa na mratibu wa kikanda cha Rift Valley, Mongo Chimwaga, aliweza kusema kuwa waliweza kutambua familia hiyo maskini.

Nakisha kuipea nyumba hiyo iliyo katika eneo la Murunyu Jimbo la Bahati.

Macharia ambaye huwa anafanya kazi ya kibarua na kulipwa chini ya shillingi 200 kwa siku moja, ana watoto sita huku watatu wakiwa ni walemavu, alisema kuwa alidhani ni ndoto kwa kupewa nyumba ya vyumba viwili vya kulala siku ya Ijumaa.

"Huwa nafanya kazi ya kibarua ili niweze kuwakimu watoto wangu, hata hivyo huwa nafanya kazi ndogo sana kwa maana huwa natumia muda wangu mwingi kwa kuwapeleka shule na kisha kuwarudisha nyumbani," Alieleza Macharia.

Mke wake wa miaka, 27, aliweza kuwaacha kwa sababu ya mzigo wa kuwalea watoto hao walemavu.

"Kwani bado naota?!mtu aweze niambia ukweli, namshukuru Mungu kwa maana ni mwaminifu,

"Niliweza kumuomba ili anifungulie njia ya jinsi ya kuwalea watoto wangu sita na kwa urahisizaidi na ameweza kutimiza ahadi yake," Alisema Macharia aliyekuwa na furaha usoni mwake.

Mwanaume huyo aliyekuwa amesaidiwa na nyumba na kanisa kwa sababu hangeweza lipa kodi yake, hangewacha kurukaruka kwa furaha  ndani ya nyumba hiyo kwa sababu maombi yake yalikuwa yamejibiwa.

"Ni kwa bahati mbaya kuwa mke wangu aliamua kuniwacha mwaka jana akisema kuwa hawezi lea watoto walemavu,

"Niliamua kubaki nyuma ili kuwalea watoto wangu kwa maana ninawapenda sana, licha ya ulemavu wao Mungu anajua kwanini ni walemavu,

"Siwezi fanya lolote kama sina watoto hawa, hata kuenda mbali siwezi enda ama kukaa siku kama sijawaona, kwa maana ni baraka na zawadi kutoka kwa Mungu," Macharia alisimulia.

Macharia hakuweza kunyamaza bali aliendelea kumsifu Mungu, huku nyumba yake ikiwa na viti, vitanda vya dhamana na kisha vyakula ambavyo ni vya pesa nyingi.

Hata watoto wake hawangeweza kuficha furaha yao kwa kitendo ambacho kilikuwa cha utu.

Nyumba hiyo ilikuwa imejengewa familia ya Dennis Ngaruiya, kijana wa kidato cha nne ambaye 2014 aliweza kukariri shairi mbele ya rais katika eneo la 3KR barracks, Lanet.

Rais hangeweza kuacha kucheka alipokuwa akikariri shairi hiyo, mama yake Dennis Damaris Wambui aliweza kukataa nyumba hiyo na wiki iliyopita na kusema kuwa, haikuwa nyumba ya kiwango ambacho Rais angetaka wapate.

"Hiyo si zawadi ambayo rais angetaka tupate mimi na kijana wangu, tena imepasuka na inakaa nyumba ambayo si ya kudumu, ilikuwa na mtu ambaye alikuwa mlemavu na kisha akahama," Wambui alisema.

Familia hiyo ilisema kuwa nyumba hiyo ilikuwa imejengwa vibaya ikilinganishwa na ile ya Martin Kamotho almaarufu githeri man aliyeonekana akiwa anakula githeri kwa kartasina kufunga foleni siku ya kupiga kura 2017.