Babu Owino akosekana mkutano wa ODM Kibra, sababu zatolewa

70651727_2594340937328929_8613079109901221888_n-2
70651727_2594340937328929_8613079109901221888_n-2
Kivumbi na mtifuano mkali wa ubabe wa kisiasa ulishuhudiwa katika eneo bunge la Kibra hapo jana Jumapili.

Raila Odinga aliongoza kikosi cha ODM huku rangi ya machungwa ikisheheni mtaa huo wa mabanda.

Raila alikita kambi uwanja wa Laini Saba huku Mariga akipiga kampeni uwanja wa Lindi.

Ushindani unaonekana wa farasi wawili katika mchakato huu wa kutafuta uungwaji mkono na kumrithi marehemu Ken Okoth.

Aidha katika mkutano wa ODM, wafuasi walitarajia kikosi chote akiwemo mbunge tata Babu Owino.

Sababu zimetolewa za mbunge huyu kutofika katika hafla hiyo iliyorindima moto jana.

Kwa mujibu wa Sifuna, Babu hakuwa anahisi vizuri kutokana na maumivu ya ugonjwa.

"Babu Owino angetamani kuwa nasi ila ikashindikana ... ni mgonjwa kwa hivyo hangeweza kufika. Lakini amesema tarehe saba atakuwa hapa kuchunga kura za ODM," Sifuna

Wafuasi walitaka kusikia kutoka wa Babu Owino ambaye huwa na maneno makali zaidi.

Ikumbukwe kuwa, mbunge aliwahi kujipata taabani kupitia matamshi hapo awali.

Aidha Sifuna alimtetea na kusema kuwa yupo na wakaazi wa eneo hili Novemba 7 katika uchaguzi huu.

Imran Okoth anatazamiwa kutwaa ushawishi mkubwa kwa watu wa Kibra ili kurithi kiti hiki.

Katika kampeni hizo, inadaiwa vijana walizua vurugu na kutupa mawe katika msafara wa ANC.

Mpaka sasa haijaweza kubainika waliohusika katika jaribio hilo la kutatiza amani.