Mtoto aliyepatikana katika shimo la choo, Ol Kalou aliachwa hapo kutoka kwengine

Mtoto aliyepatikana ametupwa katika shimo la choo katika jengo la makaazi mjini Olkalou jana jioni huenda alipelekwa hapo kutoka kwengine.

Ripoti za awali zilikuwa zimeonyesha kwamba ana umri wa mwezi mmoja lakini sasa imethibitishwa ana umri wa wiki moja.

Mwanamke anayeishi katika jengo ambamo mtoto huyo alipatikana alisema kwamba hapakuwepo mwanamke yeyote mjamzito katika jengo hilo.

Mwanamke aliyepata mtoto huyo (jina lake tumelibana kwa ombi lake), alisema kwamba alisikia kilio cha mtoto katika shimo la choo mwendo wa saa moja unusu jioni. Alimwaarifu jirani aliyethibitisha kwamba aliyekuwa akilia ni mtoto na kuitisha usaidizi.

Mtoto huyo kwa sasa anatibiwa katika hospitali ya J.M. Kariuki memorila Hospital, afisa mkuu wa matibabu katika hospitali hiyo Dkt. Joram Muraya alisema kwamba hali yake ni thabiti.

Mkaazi George Rugene alisema kwamba mtoto huyo si  wa kwanza kwa sababu watoto wengine wamepatikana wametupwa katika maeneo mengine mengi mjini Ol Kalou, na kuongeza kwanza kwamba watoto wengi wanaotupwa na wasichana.

Mkaazi mwingine, Agnes Muthoni, alionya wanawake wenye tabia kama hizo kwamba watakerwa na matendo yao siku moja.

IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO