Baraza la magavana latoa tahadhari kuhusu kuvunjwa kwa bunge

Baraza la magavana limeonya kuhusu kuvunjwa kwa bunge  kufuatia ushauri wa  jaji mkuu David Maraga kwa rais Uhuru Kenyatta .

Kupitia taarifa siku ya jumatano mwenyekiti wa COG Wycliffe oparanya amesema  ingawaje wanaelewa    msimamo wa jaji mkuu kuhusu suala hilo ,kwa sasa kutakuwa na athari  kubwa kwa taratibu za serikali endapo bunge litavunjwa hasa wakati huu ambapo serikali inapambana na janga la corona .

" Kwa sasa  taifa lipo katika mjadala wa uwezekano wa kuirekebisha taifa …huu sasa ndio wakati wa kuyazingatia mapendekezo yote kuhusu usawa wa kijinsia na kuhakikisha kwamba kanuni hiyo  inatekelezwa k iwapo marekebisho ya sharia yataafikiwa’ amesema Oparanya

Maraga  siku ya jumatatu alimshauri rais Uhuru Kenyatta kulivunja bunge  kwa kukosa kutekeleza kanuni ya usawa wa kijinsia