Bi Diana asimulia vile bwanake alitaka kumuuwa

diana-41
diana-41
Katika kipindi cha Bustani na Massawe Japanni October 19th mgeni wetu alikuwa ni dada Diana.

Diana Kamande ni nusura wa ghasia za kijamii.

Kulingana na ushahidi wake Diana aliweza kuteswa na kupigwa na bwanake, akisema alinusurika kifo.

Kama hukumbuki alikuwa katika vyombo vya habari mwaka wa 2013.

Ni mama wa watoto wawili, na kando na hayo alikumbuka ile siku alipotoka nyumbani na bwanake wakienda kazini.

Lakini la kushangaza ni yaliyotokeza baadaye.

Diana alisema;

" Hiyo siku nilimwambia bwanangu kwamba sitaweza kuenda nyumbani naye kama ilivyo desturi. Akaniandikia message kupitia simu kwamba ni sawa."

"Kumalizana na shughuli zangu nikaelekea nyumbani, na bwanangu akaniuliza chene napika usiku huo. Bwanake akasema atajishugulikia chakula ya jioni."

Bwanake alifika nyumbani usiku akiwa na hasira. "Nilishtuka kwasababu hajawahi onekana akiwa amekasirika hivyo, watot pia walishtuka. Baada ya mda kidogo alisimama na kuchukua vifunguo zote, akatoka na akafunga milango."

Na hapo ndipo mambo yalienda mrama.

Usiku wa manane alipokuwa amelala, aliamka amestuka kupata bwanake anamkata uso na kisu. Diana alivutana na mumewe hadi alipojificha chini ya kitanda.

Tazama kanda ifuatayo ya Diana akiwa ndani ya studio yetu.

&feature=youtu.be