Bila Huruma !Makau Mutua asherehekea Dennis Itumbi kufutwa kazi Ikulu

Ulimwengu huu kuna wanaokupenda na wanaokuchukia kulingana na miendneno yako au vitendo vyako .

Yaonekana Dennis Itumbi amependwa na wengi lakini pia ana  wengia mabo  hawana huruma naye . Baada ya kufutwa kazi katika wiki ambayo ilikuwa pia birthday  yake Itumbi huenda akajipata na masimango si haba mtandaoni .

Kwa mfano Profesa Makau Mutua  ametumia Twitter kuonyesha furaha yake kuhusu yaliomsibu Itumbi .Amesema ingawaje sio kawaida yake kufurahia  matatizo ya wengine , hatojibana ili kupiga tosti glasi ya kinywaji baada ya Itumbi kuonyeshwa mlango wa Ikulu.Tazama ujumbe alioandika katika twitter

https://twitter.com/makaumutua/status/1240393757763256321

Itumbi  alikuwa mkurugenzi mkuu aliyesimamia mawasiliano ya kidijitali . Nafasi nyingine zilizofutiliwa mbali ni  mkurugenzi mkuu wa mawasiliano anayesimamia  hafla , mkurugenzi mkuu anayesimamia  uandhishi wa hotuba  na afisa mkuu wa mawasiliano . Nafasi hizo nyingine zilikuwa zikishikiliwa na  James Kinyua, Erick Ng’eno, David  na  John Ndolo. Katika maelezo kumhusu katika twitter ,Itumbi amejieleza kama mfungaji wa nguruwe . Kupoteza kazi yake kumejiri wiki hii ambayo alishehekea siku yake ya kuzaliwa . Itumbi amekuwa katikati ya kesi  inayohusisha barua iliyokuwa na madai ya njama ya kumuua naibu wa rais William Ruto .