Bob Collymore aliunganisha mamilioni. Azikwa na wachache

unnamed (2)
unnamed (2)

Mdosi wa shirika la mawasaliano Safaricom aliunganisha mamilioni ya watu kupitia simu za rununu, meseji na mitandao ya kijamii na hatimaye akaikwa na watu wachache.

Pata Uhondo hapa:

Bob Collymore, 61, alichomwa jana jumanne na kuwa jivu katika hafla na kongamano la faragha. Wanahabari walizuiwa kabisa kuingia maeno yale. Msafara wa magari ulianza katika chumba cha kuhifadhi wafu cha Lee.
 Kuanzia saa 9 asubuhi, waombolezaji walianza kumiminika katika eneo la kuchoma la Kariokor. Baada ya dakika chache,viongozi na marafiki kutoka kampuni ya Safricom wakiongozwa na Nicholas Ng'aNg'a walianza kufika ili kumpa heshima zao za mwisho. Ibada ya kumpa heshima Bob inatarajiwa kufanyika kabla ya juma hili kuisha. Nafasi yake kwa sasa itazibwa na Michael Joseph ambaye atashika usukani huo kwa muda.
Pata Uhondo hapa:

Nguvu za umeme zilitumika katika zoezi nzima la kuuchoma mwili ili kuzidisha kasi ya mchakato. Collymore alizaliwa mwaka 1958 nchini Guyana na kulelewa na babu yake. Alipofikisha umri wa miaka 16 alihamia nchini Uingereza kujiunga na mamake na kusomea shule ya upili ya Selhurt.

Bob atakumbukwa kwa kupiga hatua kubwa katika kuimarisha huduma katika kampuni ya simu za rununu ya Safaricom. Aidha, kiongozi aliwajali zaidi maskini. Bob angetenga wakati wake na kuabiri gari na kutembelea watumiaji wa mtandao huu katika vitongojiduni.