Bullet Hole: Je,Kenei alijiua au aliuawa? Aliyefyatua risasi ni nani?

Risasi ilimtokea kupitia kipaji chake na uchunguzi wa mwili wake unaonyesha kwamba bunduki iliyotumiwa iliwekwa katika kidevu chake kabla ya kufyatuliwa .

Mwanapatholojia mkuu wa serikali Johansen Oduor  amesema hayo baada ya mwili wa Kipyegon Kenei kufanyiwa uchunguzi  lakini matokeo ya uchunguzi huo yamezua maswali kuliko majibu . Kifo cha afisa huyo wa polisi aliyekuwa akihudumu katika afisi ya naiu wa rais William Ruto kimesababisha shauku  ya iwapo kifo chake kilitokana na hatua yake kujiua au aliuawa .Kenei mwenye umri wa miaka 33,  alikuwa mlinzi katika jumba la  Harambee House Annex  katika ghorofa ya pili ambaypo ilitumiwa  na waziri wa zamani wa Michezo Rashid Echesa kuandaa mkutano na wanakandarasi wawili kuhusu mkataba feki ya mauzo ya silaha za kijeshi . Mwili wake ulipatikana  katika  nyumba yake ya chumba kimoja mtaani Imara Daima februari tarehe 20.

Ripoti ya polisi inaonyesha kwamba mwili wake ulipatakana na  Charles Ng’ang’a  mwendo wa saa nane alasiri baada ya kugundua uvundo uliotokea katika nyumba ya polisi huyo . Baada ya kitendawili cha kilichomuua kujibiwa na uchunguzi wa mwili wake ,swali sasa ni nani aliyefyatua risasi ? Awali maamlaka zilishikilia kwamba Kenei alijiua lakini  endapo itabainika kwamba hakujiua basi kifo chake kilitekelezwa na mtu au watu wengine na kesi hiyo itakuwa sasa ya mauaji . Kenei alitarajiwa kuandikisha taarifa na DCI kuhusu   mkutano  ambao Echesa alifanya katka afisi ya Ruto kuhusiana na mauo feki ya silahaza kijeshi za thamani ya shilingi bilioni 40 .

Alikuwa kazini siku ya mkutano huo  lakini  muda wa kifo chake unazua maswali  hususan kwa sababu alitarajiwa kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo . Familia ya Keneo imekataa kabisa dhana kwamba mwanao alijiua  lakini baadaye wamelgeza msimamo na imeripotiwa wako tayari kuamini matokeo kutoka kwa mchunguzi anayeaminika . Duru zaarifu kwamba Ruto amekuwa akiwasiliana na familia yake ili kuifariji na kuahidi kuwasaidia . Je,Kenei alijiua au  aliuawa? Iwapo aliuawa basi ni nani aliyekuwa  na sababu ya kumuua?