BUNGOMA: Jamaa Amfungia Mkewe Na Kumteketeza Kwa Kuchelewa Kumpakulia Nyama

bungoma
bungoma
Polisi huko Bungoma wanamsaka mwananaume mmoja mwenye umri wa miaka 34 kutoka mtaa wa Ten star viungani vya mji wa Bungoma anayesemekana kumfungia mkewe nyumbani na kumteketeza kwa tuhuma za kuchelewa kumpa chakula cha jioni.

Mshukiwa Onyango Ooko ambaye alienda mafichoni siku nne zilizopita baada ya unyama huo anasemekana kumchoma mkewe kwa kutumia jiko muda mfupi tu baada ya ugomvi baina yao.

Onyango anadaiwa kufika nyumbani akiwa mlevi akampa mkewe kipande cha nyama alichotaka kupikiwa na baada ya muda mchache subira yake ikakosa heri na kumchoma mkewe na jiko iliyokua ikianda chakula hicho.

Mhadhiriwa alikimbizwa katika hospitali ya Khalaba alipofariki akipokea matibabu.