Bungoma: Polisi Wamsaka Mama Aliyeiba Mtoto Wa Siku Tano

Polisi kaunti ya Bungoma wanamsaka mama moja anayeshukiwa kumwibia mwenzake mtoto mchanga msichana wa siku tano ambaye hakuwa hata amepewa jina.

Philis Nanjala kutoka Chwele eneo bunge la Kabuchai amesema mwanawe aliibiwa katika hospitali ya rufaa ya Bungoma alipokuwa amempeleka kwa matibabu na ndipo alimwachia mama mmoja amchungie, muda mfupi aliporejea baada ya kwenda msalani akapata mwanawe ametoweka na mama huyo ambaye sasa ameingia mafichoni na hajulikani aliko.

-Brian Ojamaa