Kabla sijamzaa Dylan niliwahi kuwa mjamzito mara 3 lakini zikatoka-Hamisa Mobetto

Muhtasari
  • Nilibeba miba tatu za Diamond huku zikitoka mapema
  • Diamond aliuliza tukafanyiwe DNA kuhakikisha kama Dylan ni wake
Hamisa 2
Hamisa 2

Hamisa Mobetto kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu ujauzito wake, huku akiwa kwenye mahijiano na wasafi Fm alisema kwamba alibeba mimba tatu za msanii Diamond huku zikitoka mapema.

Hamisa pia alisema kwamba mwanawe Dylan ni wa mimba yake ya nne, mimba ya kwanza ilitoka alipokuwa ameenda safari ya nchi za ng'ambo na msanii huyo.

Alieleza na kusema kuwa kupitia ujauzito wake Dylan amekuwa na Diamond wakati huo wote hadi pale alienda kujifungua.

Huu hapa usimulizi wake;

“Kabla sijamzaa Dylan niiwai kupata ujauzito, three pregnancies ambapo nilipata ujauzito wa kwanza ulitoka, tulisafiri sijui tunaenda nchi gani mimba ikatoka bahati mbaya. Nikaja nikapata ya pili, ikatoka, ya tatu ikatoka. Ni period ambayo tulikuwa Pamoja. Dylan alikuwa mimba ya nne so tulikuwa wote na ujauzito wote tulikuwa Pamoja mpaka siku ambayo mimi naenda kujifungua. Kwa hiyo I feel like kama kuna binadamu alikuwa na uhakika kwamba ule mtoto ni wa kwake, basi yeye ni number moja." Aliongea Hamisa.

Pia alifichua kuwa Diamond alisihi ili waweze kufanyiwa DNA ili kuhakikisha kuwa Dylan ni mwanawe kamili.

“Tukaenda tukapima DNA nadhani walichukua vipimo vinne kila mtu (mama, baba na mtoto) tukasign pale ivo wakasema tusubirie sijui ni 2 or 3 weeks so tukasubiria majibu yakatoka mtoto akatoka kwa asilimia zote ni mtoto wake na ikaishia hivyo. Na kwa kweli wakati tunaelekea hospitali alikuwa anajiskia vibaya. It was very sad for me to watch as a mother kwa sababu as a mother ni mimi natakiwa nijiskie vibaya."

Hamisa alisema kwamba alifanya hayo ili kukomesha uvumi kuwa Dylan si mwanawe Diamond.