Mamake Diamond na dadake Esma wawashambulia Hamisa,Tanasha

Diamond Platinumz
Image: File
Familia  ya Diamond Platnumz imeamua kufungua vijembe na vita vya mameno kwa wapenzi wote wa zamani wa msanii huyo .

Mamake Sandra na dadake Esma  huenda ndio kikwazo kikubwa kwa mwanamuziki huyo kudumu katika mahusiano na wanawake wengi ambao amewahi kuhusishwa nao na hata kuzaa nao watoto .

Nyota huyo ametoa wimbo kwa jina Haunisumbui,  unaoonekana kuw ana ujumbe foche kuwalenga Hamisa Mobetto na Tanasha

Unasema hivi wimbo huo ;

Si ko ko si kanda mbili yani vyote

Haviku pendezi kuwa na ngoko

Usio nawiri tope niutelei

Utaishia kututabiri

Tubomoke ina songa miezi

Mola amesha taka dhiri usijichoshe

Haivunjiki penzi

Hazikukai mascara wala makeup zina kushuka uso ume ku parara

Zingetenguka uso sauti yastara kwa kudeka

Una weuke jibwa koko la mbagala

ina bweka na kubwetuka wala

Wala hunisumbui wala

Wengi wamelitafisiri hilo kama kijembe cha moja kwa moja kwa wapenzi wake hao wa zamani kwa tabia zao. Dadake Diamond Esma aliutuma wimbo huo na maneno haya;

TOBA TOBAAA SASA MAEX ZETU SI WATATUCHAMBA TUKOME TUITWE KUNGURU NA MAKEUP ZETU ZA KUTUSHUKA NA USO UMETUPARARA… ALAFU KUTWA KWA MAPAGE FAKE KM @JUMALOKOLE2

Mamake alijibu kwa kusema

 HAIYA WALE WATEGEMEA MAKEUP OOOYOOOOO.

Watumizi wa mitandao ya kijamii nao hawakunyamaza na majibu yao kwa drama hiyo ilikuwa kama hivi ;

samlucksamadizo Hiii familia kweli mediocres

mamak_eshania Mediocres yaani kumbe pia wanaume hujua kuchamba waaah… This is new… Unachamba mwanamke umewaijifunika naye blanket and you think karma itakuspare

witnessjustus Tabu ya kudate na waswahil utaimbiwa taarabu paka bas pole kwa ma X wote wa huyo mtandale