'Ukiulizwa sema hujui ni ugonjwa upi unanisumbua,'Mcheshi Kasuku azungumzia nyakati zake na Othuol

Muhtasari
  • Othuol angefufuka ningemwambia tuachane na pombe na tuende kanisani
  • Wakati ambao sitawahi sahau nikiwa na Othuol ni pale tulishikwa na polisi na kujifanya kuwa ana ugonjwa wa kifafa ili tuachiliwe
Othuol Othuol

Baada ya kifo chake mchekeshaji wa churchill Show Othuol kufahamika sana wacheshi wenzake walimuomboleza kama mtenda kazi na mwenye mawaidha mapya ya kazi yake.

Huku mchekeshaji Kasuku akiwa kwenye mahojiano akimuomboleza mwendazake alizungumzia nyakati ambazo walikuwa pamoja na Othuol kabla ya ugonjwa wake na kifo chake.

"Kuna wakati ambao sitawahi sahau nilikuwa na Othuol na tukashikwa tukienda South B tukapelekwa katika kituo cha polisi cha Industrial area 

Othuol aliniambia Kasuku nyamaza tu tukaingizwa kwa jela akaniambia wewe sema tunafanya kazi kwa muindi na hujaniona kwa muda mrefu na ulikuwa umekuja kunichukua kwa nyumba na hujui ni nini inanisumbua, hujui ni ugonjwa upi unanisumbua." Alieleza Kasuku.

Kasuku alileza jinsi waliachiliwa kutoka jela baada ya Othuol kufanya drama,

"Ikafika saa kumi Othuol alikanyaga kila mtu kwa jela ni kama alikuwa na kifafa kila mtu alitawanyika na kuniacha ni msaidie afisa wa polisi aliingia kwa seli na kuuliza huu ni ugonjwa upi

Ilikuwa inafurahisha nilijua tu alikua anaigiza, alinifinyia jicho akaanza kugonganisha kichwa kwa sakafu

polisi wote waliingia kwa selo na kuuliza alikuwa na nani nikasema ni mimi, walianiambia peleka huyu kijana nyumbani

Tulipopita lango kuu aliniambia niachilie mimi si mgonjwa bwana."

Kasuku alisema ya kwamba Othuol angefufuka leo angemshauri waokoke na waachane na pombe kabisa.