'Nitasema ukweli kuhusu DJ Mo na mimi,'asema mwanamke aliyedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye

Muhtasari
  • Tarehe 1 Novemba nitasema ukweli kuhusu hadithi ya DJ Mo
  • DJ Mo na Size 8 walisamehana baada ya drama yao ya Mo kutoka nje ya ndoa
Margaret Wanyama ,mwanamke aliyedai kuwa katika uhusiano na DJ Mo

Ndoa ya Size 8 na DJ Mo imepitia majaribu katika siku chache zilizopita baada ya Margaret Wanyama kujitokeza na madai kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na DJ Mo.

Kila jambo linaonekana kurudi kwa nafasi yake kwa maana baada ya drama hiyo yote  mcheza santuri Dj Mo na Size 8 walienda kujivinjari ili kusheherekea ndoa yao, lakini inaonekana ndoa ya wawili hao haitakuwa na furaha baada ya tarehe moja Novemba mwaka huu.

Hii ni baada ya Margaret kusema ya kwamba tarehe hiyo atasema ukweli kuhusu drama yake na Mo.

Kupitia kwenye mtandao wake wa kijamii wa instagram Margaret alikuwa na haya ya kusema,

"Kama wataka kujua ukwei kuhusu drama ya DJ Mo nitakuwa moja kwa moja tarehe 1 Novemba nitasema ukweli kwa upande wa hadithi yangu." Aliandika Margaret. 

Haya basi wacha tungoje siku hiyo kuangalia nini atakachosema haswa kuhusu uhusiano wake wa Dj Mo.