Wayne Rooney astaafu kama mchezaji, ateuliwa kuwa kocha wa Derby County

wayne rooney ateuliwa kama meneja wa Derby County
wayne rooney ateuliwa kama meneja wa Derby County

Klabu ya daraja la pili  Derby County imemtaja mfungaji bora wa Uingereza, Wayne Rooney kama kocha mkuu kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.  

Rooney mwenye umri wa miaka  35 amekua akihudumu kama kocha wa muda baada ya kocha mkuu Phillip Cocu kuchujwa Novemba  tarehe 14. Rooney sasa amestaafu rasmi kutoka soka, na atapambana kuwaepusha  vijana wake na shoka kwani wanashikilia nafasi ya 22  kwenye jedwali.

Kiungo wa  Manchester United Bruno Fernandes jana alitajwa kama mchezaji bora wa ligii ya EPL wa mwezi Disemba.  Fernandez sasa ameshinda taji hilo mara nne msimu huu na kufikia rekodi ya wachezaji wa zamani Paul Scholes na  Cristiano Ronaldo  ugani Old Trafford . Fernandez amesalia na taji  moja la mcheaji bora  wa mwezi nchini  Uingereza ili kufuikia rekodi ya   washambulizi wa zamani Wayne Rooney na Robin van Persie.

 Mshambulizi wa  Ulinzi stars Enosh Ochieng atakosa mechi za ligi kuu nchini kwa miezi mitatu, baada ya kuondoka  kufanya masomo zaidi ya kijeshi. Ochieng ambaye  ni mwan jeshi alinyakua taji la mfungaji bora katika ligi mwaka wa 2018, na kocha mkuu Dunstan Nyaudo anadai watazikosa sana huduma zake. Ochieng ni mmoja wa wachezaji ambao wanakwenda kwa  masomo zaidi kama ilivyo desturi ya kikosi hicho cha Nakuru.