'Mungu amefanya zaidi ya mawazo yangu,'Size 8 azungumzia jinsi Mungu aliokoa mwanawe

Muhtasari
  • Size 8 azungumzia jinsi Mungu aliokoa mwanawe alipokuwa hospitalini baada ya kujifungua
  • Pia aliwashauru mashabiki wake wasiweze kukata tamaa ata kama hali ni ngumu kiasi gani
Muraya-ladasha-size-8-mpasho
Muraya-ladasha-size-8-mpasho

Msanii wa nyimbo za injili Size 8 kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amekumbuka jinsi Mungu aliokoa maisha ya mtoto wake baada ya kujifungua.

Kupitia kwenye ujumbe wake msanii huyo alisema kwamba Mungu amemtoa mbali ndio maana huwa anamuabudu kila wakati.

Pia aliwashauru mashabiki wake wasiweze kukata tamaa ata kama hali ni ngumu kiasi gani.

 

"Mungu UMETENDA makuu huyu alikuwa @muraya.jnr siku za kwanza ospitalini huko ICU nilimkaribia kumpoteza madaktari wa usiku wa tatu walimzunguka wakijaribu kila awezalo kuokoa maisha yake na Yesu Kristo akiwa hai ndani yangu alifanya muujiza na mtoto wangu hakufa.

Unaniona nikimsifu Mungu kila wakati kwa kuwa amefanya zaidi ya mawazo yangu !!! Mimi si kitu bila Mungu 😭😭😭😭.

Kamwe usimkate tamaa Mungu hata hali yako iwe ngumu kiasi gani. NASHUHUDIA MUNGU KILA SIKU. Inama na kuabudu," Aliandika Size 8.