Sikujua Samidoh alikuwa ameoa, hakuwa na pete,'Karen Nyamu asema hakumchanganya msanii huyo

Muhtasari
  • Karen Nyamu asema hakufahamu Samidoh alikuwa ameoa

Mwanasiasa Karen Nyamu kwa mara ya kwanza amezungumza kuhusu uhusiano wake na msanii wa kikuyu Samidoh.

Akiwa kwenye mahojiano na Bonga na Jalas alidai kwaba hakumchananya msanii huyo kwani hakujua ameoa kwa maana hakuwa na pete kwenye kidole chake.

Karen alivuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya Samidoh kuomba msamaha kwa mashabiki na kumtambulisha kama rafiki na wala si mpenzi.

"Ni muhimu sana kuweka mambo wazi,sipendi jinsi mambo yamwekwa,siombi msamaha,mimi sio mjinga, napenda kuishi kwa ukweli

ikiwa ukweli wangu ni mgumu ndio ukweli wangu ,ninapenda kuwa mkweli,tulipatana na Samidoh katika hafla ya kisiasa na tukakuwa marafiki

Sikujua kwamba Samidoh alikuwa ameoa, kwani hakuwa na pete, nilikuja kuhua ameoa baada ya miezi 4

Niliambiwa na mwakilishi wadi mafirifiri," Alisema Karen.

Alizidi na kueleza upande wa hadhithi yake na jinsi alijipata akiwa na Samidoh, na kuwa hakutaka kuvunja ndoa yake,

"Sitaki kuonekana mtakatifu,tatizo ambalo ninalo ni kwamba watu wananiona kama mimi ni mvunja familia 

Na nilitaka kuunja familia ya Samidoh na kutaka kushindana na mke wake,"