Mke wangu amekuwa akibugia vileo sana na kuniachia majukumu ya nyumbani,'Mwanamume alia

Muhtasari
  • Hawakukosea waliposema kwaba kama umeamua kuingia katika ndoa unapaswa kuvumilia mambo yote kwani ndoa sio mchezo wa paka na panya
  • Mwanamume mmoja alisimulia yale amekuwa akipitia katika ndoa yake

Hawakukosea waliposema kwaba kama umeamua kuingia katika ndoa unapaswa kuvumilia mambo yote kwani ndoa sio mchezo wa paka na panya.

Kuna wale wanaume ambao hudaiwa wamekaliwa chapati na wake zao kwa kufaya yale yote wake zao huwaambia wafanye.

Ndoa za wakati wa sasa hazidumu kwa sababu wengi huwa hawajaamua kuvuka upande huu mwingine.

Mwanamume mmoja alisimulia yale amekuwa akipitia katika ndoa yake.

Huu hapa usimulizi wake;

"Mke wangu amekuwa akibugia vileoa sana, akienda kazi akirudi nyumbani anarudi akiwa amelewa

nimekuwa nikifanya majukumu yote ya nyumbani, huwa napika, nabadilisha mtoto 'pampers' nikimwambia abadilike anasema kwamba nina mpango wa kando

Amepata kazi mwaka huu, sasa anataka nifanye yote ambayo ananiambia, hata hataki nisimame wala kusalimia mtu mahali tunaishi

Kwa sasa nimetoka nyumbani ili nimpe muda afikirie, mimi nafanya kazi ya bawabu," Alieleza Mwanamume huyo.

Je ni mambo yapi ambayo umekuwa ukipitia katika ndoa yako ilhali umenyamza ili kuokoa ndoa yako?