Mbwa wangu ana wafuasi wengi mitandaoni kuwaliko-Wema Sepetu awaambia wakosoaji

Muhtasari
  • Kwa siku chache zilizopita Wema alipakia picha ya mbwa wake na kutangaza kwamba amepotea na mu atakaye mpata ata mpa elfu mia moja pesa tasilimu za Tanzania

Muigizaji Weam Sepetu kupitia kwenye ukurasa wake wa instagrama amewakosaoa mashabiki na wakosoaji wake ambao wanakejli mbwa wake.

Kwa siku chache zilizopita Wema alipakia picha ya mbwa wake na kutangaza kwamba amepotea na mu atakaye mpata ata mpa elfu mia moja pesa tasilimu za Tanzania.

Muigizaji huyo alieleza jinsi mbwa wake alipotea.

"Naona comments nyingi.... Bado sijampata jamani.... Labda tu nielezee jinsi alivyopotea....

Mimi naishi karibu na Kigamboni na kila siku gari ya Production huja mpaka nyumbani na kunichukua kwa ajili ya Kwenda Location...

Juzi ilivyokuja nikawa sijaingia kwenye gari cause nilikuwa sina Scenes za kushoot so I told the driver aende tu kuwapitia watu wengine Kambini.... Kwa hivyo kilichotokea since Vanilla ameshazoea naendaga nae location without her knowing gate lilivyofunguliwa kuruhusu gari litoke,

mbwa nae akaanza kufata gari, kaikimbiza na mpaka sasa sijui bado kama aliikimbiza mpaka wapi, ni majirani tu ndo wamesema kuwa alikuwa anakimbiza gari.... So thats the story... Sijui bado kama mbwa wangu yupo hai au amekufa...." Aliandika Wema.

Pia alisema kwamba mbwa wake yuko na wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijami, kulio wale ambao wanamkejeli.

Wema alimuomba kama kuna mtu ambaye alimchukua amtunze na wala hasimtese.

"Kuna wapuuzi wanasema kuwa namtafutia ustar.... Vanilla is already a Star jamani.... Page yake tu ina 15K followers.... Wengi wenu hata hao 15K hamna... So tusikerane zaidi.... My baby is still Lost na nahitaji kumpata.... Pia kama ametekwa huko basi jus make sure mnampa mahitaji yake sio mnanitesea mtoto.......Bado hajapatikana... Still looking....🥺🥺🥺,"