Msanii ninayempenda na bora ni Solomon Mkubwa-DP Ruto afichua

Muhtasari
  • Naibu William Ruto akiwa kweye mahojiano alizungumzia mambo kadha wa kadha, kuhusu chama cha JUbilee na UDA
  • Pia alizungumzia maisha yake, huku akisema kuwa anampenda msanii wa nyimbo za injili Solomon MKubwa
Naibu rais William Ruto akizungumza katika kanisa la House of Hope mtaani Kayole siku ya Jumapili, Januari 10, 2021.
William Ruto Naibu rais William Ruto akizungumza katika kanisa la House of Hope mtaani Kayole siku ya Jumapili, Januari 10, 2021.
Image: DPPS

Naibu William Ruto akiwa kweye mahojiano alizungumzia mambo kadha wa kadha, kuhusu chama cha JUbilee na UDA.

Pia alizungumzia maisha yake, huku akisema kuwa anampenda msanii wa nyimbo za injili Solomon MKubwa.

Huku akizungumzia chama cha siasa cha Jubilee alikuwa na haya ya kusema,

 
 
 
 

"Pale chama cha JUbilee mimi ni naibu mwenyekiti, lakini kwa bahati mbaya kimetekwa nyara, kama JUbilee itaendelea kubomolewa tutajiunga na UDA na safari itaenddelea

Watu wwameweka katika akili zao kwamba tuna msafara wa kushinda na kushindwa, lakini hawajui kwamba kuna msafara wa kushinda kushinda

Wapinzani wangu hawawezi leta pamoja wabunge 140, kama vile mimi nilikuwa na mkutano wa wabunge 140," Aliongea Ruto.

Alipoulizwa anampenda msanii yupi alisema haya,

"Napenda msanii Solomon MKubwa na napenda wimbo wake wa 'Mungu mwenye nguvu' napenda Nyama Choma and Mahindi Choma pia hapo niko kabisa," Alijibu Ruto.

Licha ya kigogo huyo kuwa mfano mwema kwa wakenya, alisema kwamba kuna vitu ambavyo anapeza, kando ya kuwa kiongozi.

"Window-shopping- hii window shopping unajua pale tu hii kuangalia, iko kitu Fulani pale, kuna new style hapo ya viatu, sijui nini pale

 
 

Hiyo window shopping ni kazi mzuri sana lakini sai haiwezekani. Watu wengi watazusha ama itabidii nivae miwani na sijui ni hapo

Maisha ni panda shuja, tia bidi, pole pole utafika, na Vijana muache presha nyingi bana, stress itawamaliza," 

DP alisema kwamba ni rafiki wa rais wa karibu na wametoana mbali na anaheshimu jinsi anaamua kufanya kazi.

To Subscribe To PichaClear Youtube Channel Click this link https://www.youtube.com/pichaclearfilms #BongaNaJalas https://jalangotv.com/