'Akaunti yangu ya Instagramu ni ya Diana,' Bahati atangaza

dm
dm

Kama umekuwa ukipekua pekua mtandao wa kijamii wa Instagram wake msanii maarufu, Bahti, basi utagundua kuwa asilimia kubwa ya picha zilizochapishwa mle ni za mkewe, Diana Marua.

Diana ni mojawapo ya watu wachache mashuhuri ambao hawana haya ya kuchapisha picha za wake au wapendwa wao mara kwa mara.

Huku wengi wakificha nyuso za wapenzi wao, Bahati huhakikisha kuwa sura ya mkewe Diana imerembesha mtandao wake kama jinsi ua hufanya mazingira.

Kwa hilo, msanii huyo alitangaza rasmi kuwa akaunti yake sasa ni kama ya pili ya Diana, licha ya mkewe kuwa na mtandao wake wenye wafuasi milioni 1.6.

Huku akichapisha picha nyingine maridadi ya Diana, Bahati aliandika;

Natangaza rasmi kuwa akaunti hii ya IG ni akaunti ya pili ya mke wangu. Idadi ya nyakati ninazochapisha picha zake hazifikii zangu aki ng'aa Signora Bahati, mama wa watoto wangu. Nimebarikiwa kuwa na wewe maishani mwangu.