'Familia yangu ni mashujaa wangu,'Muigizaji wa Mother-in-law Mustafa asema baada ya kuachwa na marafiki

Muhtasari
  • Muigizaji Andrew Muthure maarufu Mustafa akiwa kwenye mahojiano alifichua kwamba amekuwa akisaidiwa na familia yake baada ya kupoteza kazi yake
  • Pia alifichua kwamba alipoteza kazi wakati mke wake alimuhitaji sana kwa maana alikuwa na ujauzito wa miezi 

Muigizaji Andrew Muthure maarufu Mustafa akiwa kwenye mahojiano alifichua kwamba amekuwa akisaidiwa na familia yake baada ya kupoteza kazi yake.

Pia alifichua kwamba alipoteza kazi wakati mke wake alimuhitaji sana kwa maana alikuwa na ujauzito wa miezi 5.

Baada ya muigizaji huyo kuachishwa kazi familia yake imeweza kumsaidia kwa mudaa wa zaidi ya mwaka mmoja, alifichua.

"Wakati niliachishwa kazi mke wangu alikuwa na ujauzito wa miezi 5, Familia yangu imekuwa mashujaa wangu kwani wamekuwa wakinipa ushauri, kuniletea chakula na hata kunilipia kodi ya nyumba

Nina fanya kazi ya ukulima nyumbani, lakini familia yangu inanisaida kwa sababu sina kazi, hata wakati mwingine nalipa kodi ya nyumba kidogo kidogo, lakini habari nzuri ni kuwa nina mwenye nyumba mzuri sana," Alisimulia MUstafa.

Pia aliichua kwamba marafiki walimtoroka baada yake ya kupoteza kazi.

Mustafa alidai marafiki hao akiwapigia simu hawapokei wala kumpigia anapowaambia kwamba anahitaji kazi.

Kupitia hayo yote muigizaji huyo alisema kwamba amesoma mambo na jinsi ya kuongoza akili yake na roho yake.