Waliongoja kifo Changu nataka kusema Niko mzima-Msanii Syokau

Muhtasari
  • Msanii wa nyimbo za injili Justina Syokau amekuwa akivuma baada ya kujitokeza na kusema anataka msaada wa matibabu baada ya kuwa mgonjwa
Justina Syokau

Msanii wa nyimbo za injili Justina Syokau amekuwa akivuma baada ya kujitokeza na kusema anataka msaada wa matibabu baada ya kuwa mgonjwa.

Syokau awali amekuwa akipitia changamoto, na kejeli nyingi kutoka kwa mitandao ya kijamii.

Baada ya kejeli hizo, msanii huyo kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook, alipakiavideo na kusema kwamba amewasamehe wale wotw ambao walimtusi na kumsemea mabaya.

Pia aliwashukuru mashabiki wake na wale wote ambao wamemshika mkono na kumsaidia,alisema kuwa na ploti lakini hawezi uza kwa bei ya chini kwa maana anahitaji msaada.

"Bwana asifiwe, Mungu awabariki kwa kunishika mkono, asanteni kwa maombi yenu, nimeona watu wakisema na kutoa maoni kwamba natapeli watu

Kuna wale wanasema nifariki,lakini siwezi kufa kwa sasawale wote walinitusi nataka kuwaambia kwamba nimewasamehe

Kama mtu ni mgonjwa na humpendi haya basi usijaribu kumwamndikia matusi kwa maana hujui nini wanapitia, kama hunipendi usiandike kitu mbaya ama wacha kuwa shabiki yangu," Alisema Syokau.

Pia aliweka wazi kwa wale waliotaka, afe kwamba yuko hai na ataamka tena kwa jina la yesu.

"Walio ngoja kifo Changu nataka kusema Niko mzima kabisa na naedelea kupona, kifo sio dawa yangu katika jina la yesu

Nitaamka tena katika jina la yesu kristo," Aliandika Justina.

Ni ujumbe ambao wanamitandao walisema kwamba ulikuwa unamwendea au waendea wote ambao walitaka msanii huyo afe, Justina alifahamika sana baada ya kutoa kibao chake cha ''2020'