Mke wangu aliniacha kwa maana nilikuwa mraibu wa kucheza kamari-Mwanamume asimulia

Muhtasari
  • Jamaa asema aliachwa na mkewe kwa ajili ya kucheza Kamari
  • Kuna wale husema yametosha na kukata tamaa ya kuwa kwenye ndoa tena

Sababu kuu ya kumuacha mume wako au mke wako ilikuwa ipi, baadhi ya wanandoa huvumilia kwa muda mateso ambayo hupitia kwa ndoa.

Kuna wale husema yametosha na kukata tamaa ya kuwa kwenye ndoa tena.

Mwanamume mmoja aliwaacha mashabiki wa radiojambo midomo wazi baada ya kupena sababu ambayo mke wake alimuacha.

"Nilikuwa na mke na tulikuwa tumebarikiwa na mtoto mmoja, aliniacha baada ya kuniambia kwamba naharibu pesa zangu

Alianiachia mtoto, ndio nakubali nilikuwa mraibu wa kucheza kamari, lakini zaidi ya yote nilikuwa natimiza mahitaji ya nyumbani

Nikimpigia simu arudi alikataa, na kuniambia nibadilishe tabia, lakini sioni kama naweza acha kucheza kamari kwa maana namtimizia mahitaji yake yote," Alisimulia.

Kuna baadhi ya watu ambao hupitia mateso mengi kwenye ndoa lakini wanag'ang'ana na kutatua shida zao lakini mwanamke huyo alifanya vyema kumuacha mwanawe na mume wake licha yake ya kuwa baba yake.

Ni mambo yapi ambayo ulipita kwenye ndoa na kusema kuwa yametosha hutaki mambo ya ndoa tena?

Na je mwanamume huyo alijuta kuwa mraibu wa kamari, na kuamaua kmrudia mkewe baada ya kubadiilika?