(+Picha) Nyota ya 'Ugali man' yaendelea kung'aa

Charles Odongo almaarufu kama 'ugali man' ametunukiwa shilingi milioni tano na gari mpya na kampuni ya kamari

Muhtasari

•Video yake akikula ugali kwa ari kubwa ilisisimua mitandao wiki kadhaa zilizopita

•Amezinduliwa kama balozi wa Odibets

Charles Odongo akipokea cheki ya Sh5,009,000
Charles Odongo akipokea cheki ya Sh5,009,000
Image: Hisani

Nyota ya Charles Odongo almaarufu kama ‘Ugali man’ man inaendelea kung’aa baada yake kupokezwa donge nono la pesa na gari jipya na kampuni ya kamari ya Odibets.

Odongo alitangazwa kuwa balozi rasmi wa kampuni hiyo siku ya Jumanne kwenye hafla iliyofanyika katika hoteli ya Sarova Stanley, Nairobi.

Odongo ambaye alipata umaarufu mkubwa wiki kadhaa zilizopita baada ya video yake akikula ugali kwa ari kubwa kuenea mitandaoni alitunukiwa Sh5,009,000 na gari jipya aina ya VOXY.

Pesa alizopewa ‘Ugali man’ zilikuwa za kuinua kazi yake ya mazoezi ya viungo pamoja na kutunza paka wake almaarufu kama ‘puss puss’.

Akipokea zawadi hilo, Ugali man alisimulia namna alipoteza kazi yake kufuatia janga la Korona na kuahidi kusaidia wengine walio kwenye shida.

Vile odibets wamenishika mkono, pia mimi nitakuwa nashika wengine mkono” Odongo alisema.

Tazama hapa picha za hafla hiyo.