"Usikubali kupata ujauzito kama hujui anaishi wapi" Nadia Mukami ashauri wanadada juu ya mahusiano

Mukami amewashauri watu kuchumbia watu ambao wanajivunia kuwa nao.

Muhtasari

•Kupitia ujumbe wa kushauri ambao alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Mukami amesema kuwa kuchagua baba au mama mzuri wa watoto wa yeyote ni muhimu kushinda kuchagua mke ama mume.

Nadia Mukami
Nadia Mukami
Image: Instagram

Mwanadada mwanamuziki tajika nchini, Nadia Mukami ameshauri wanawake jinsi ya kuchukulia mahusiano.

Msanii huyo mwenye umri wa ujana amewasihi wanadada kuwa makini wanapojitosa kwenye dimbwi la mapenzi.

Kupitia ujumbe wa kushauri ambao alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Mukami amesema kuwa kuchagua baba au mama mzuri wa watoto wa yeyote ni muhimu kushinda kuchagua mke ama mume.

Mukami amewashauri watu kuchumbia watu ambao wanajivunia kuwa nao.

"Chumbia mtu ambaye anaringa nawe. Kuna tofauti kati ya uhusiano wa kibinafsi na uhusiano ambao umewekwa siri" Mukami alisema.

Amewashauri ambao wanapanga kuwa kwenye uhusiano kuepuka watu ambao bado wamekwama kwenye mahusiano yao ya awali. 

Mukami pia ameshauri kina dada kutahadhari dhidi ya kupata ujauzito wa mwanaume ambaye bado hawajajua mahali anaishi.

"Usikubali kupata ujauzito wa mwanaume ambaye hujui anakoishi!!

Mwanaume au mwanamke ambaye hawezi kununulia angalau kikombe cha kahawa cha shilingi mia tu wakati mnachumbiana hatawahi kununulia zawadi yoyote hata mkioa

Mpenzi wako anafaa kuwa wa kwanza kusherehekea ushindi wako kwa mfano; kuhitimu, kufungua biashara, kuinuliwa hadhi n.k. Mpenzi ambaye hasherehekei ushindi wako hafai" Mukami aliandika.

Hapo mwezi wa Mei, Mukami alifichua mwanaume mwenye asili ya Kihindi aliyemtambulisha kama Priyan kama mpenzi wake kupitia mtandao wa Instagram. Aliambatanisha picha yao wawili na ujumbe ambao uliashiria kuwa wanachumbiana.

"Licha ya yote ambayo wamesema kufikia leo, umenionyesha mapenzi tele na nik hapa natabasamu kando yako. Ukiwa mtu anayeonekana sana unahitaji mtu ambaye anakupenda. Mtu ambaye anaona zaidi ya umaarufu, pesa, uvumi, matusi na kudhalilishwa.

Mtu ambaye anazungumza na nafsi yako na wewe uko hivo. Natamani ningekujua mapema niweze kupata mapenzi ambayo unanipata, hata hivyo sijachelewa. 

Tumetoka jamii mbili tofauti lakini mapenzi yetu yanakuja mbele.

Nakupenda sana Priyan" Mukami aliandika chini ya picha yake na Priyan.

Mukami alimshirikisha mhindi huyo kwenye video ya wimbo wake 'Nipe Yote'. Hata hivyo, hajaonekana tena akizungumzia uhusiano wake na Priyan tangu kutolewa kwa wimbo huo.