Wapenzi Hamo na Jemutai waazimia kujenga nyumba pamoja baada ya kununua shamba

Tangazo lao la hivi karibuni limeashiria kuwa wawili hao wako na mpango wa kujenga nyumba na kuileta familia pamoja.

Muhtasari

•Licha ya changamoto zilizokumba mapenzi yao miezi michache iliyopita wacheshi Profesa Hamo na Jemutai wameendelea kupiga hatua kubwakubwa katika juhudi za kuimarisha ndoa yao.

•Ni dhahiri kuwa hata baada ya kutumbuiza Wanamitandao na drama za mapenzi wacheshi hao wawili waliweza kusuluhisha mzozo uliokuwa baina yao na kwa sasa wako tayari kupeleka uhusiano wao kwenye hatua nyingine.

Image: INSTAGRAM//JEMUTAI

Licha ya changamoto zilizokumba mapenzi yao miezi michache iliyopita wacheshi Profesa Hamo na Jemutai wameendelea kupiga hatua kubwakubwa katika juhudi za kuimarisha ndoa yao.

Tangazo lao la  hivi karibuni  limeashiria kuwa wawili hao wako na mpango wa kujenga nyumba na kuileta familia pamoja.

Kwenye kurasa zao za Instagram wapenzi hao walipakia picha ya selfie ambapo walionekana kujawa na bashasha kweli huku Jemutai akiwa ameshika hatimiliki ya ardhi mikononi kisha kuiambatanisha picha ile na jumbe za kueleza furaha yao.

"Ona Mungu.. Shukran, moyo wangu umeridhika. Acha tujenge nyumba sasa" Jemutai aliandika kwenye ukurasa wake.

Hamo kwa upande wake alisema kuwa ingawa hapo awali uhusiano wao umekabiliwa na changamoto si haba, hatua ya kununua shamba ilikuwa mwanzo tu wa kazi inayoendelea na anatazamia kuleta familia yake pamoja ili kuishi kwa furaha.

"Najua tumepitia mengi ila haijalishi tulivyoanza ila tutakavyomalizia. Ilikuchukua muda kuamini kuwa nilitaka familia yangu kuwa pamoja na kuishi kwa furaha, hiyo ni kazi ambayo inaendelea na huu ni mwanzo tu. Naweza kujengea nyumba bila shaka utaifanya kuwa nyumbani " Hamo aliandika.

Kwenye mtandao wa YouTube wawili hao wamekuwa wakisimulia safari ya mapenzi yao kwenye kipindi wanachoita 'Raw & Candid.

Ni dhahiri kuwa hata baada ya kutumbuiza Wanamitandao na drama za mapenzi wacheshi hao wawili waliweza kusuluhisha mzozo uliokuwa baina yao na kwa sasa wako tayari kupeleka uhusiano wao kwenye hatua nyingine.

Wanamitandao wameendelea kuwapongeza kufuatia fanikio la kununua shamba.